Halmashauri ya Mji wa Kahama Mkoani
Shinyanga imekusudia kuifikisha mahakamani, kampuni ya Vumilia Producers
Shoping Center inayosimamia soko la wakulima kutokana na kuvunja sheria ya
halmashauri hiyo baada ya kuanza ujenzi wa soko hilo bila kibali.
Kaimu
mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mji wa Kahama, Michael Nzingula alisema
hatua hiyo wameifikiwa baada ya kampuni hiyo kukaidi agizo la halmashauri
ya...
kuwataka wafanyabiashara kuondoka katika soko hilo na kuhamia kwenye masoko yanayomilikiwa na halmashauri.
kuwataka wafanyabiashara kuondoka katika soko hilo na kuhamia kwenye masoko yanayomilikiwa na halmashauri.
Alisema kwa sasa wamepeleka
zuio la kusitisha ujenzi wa vibanda katika soko hilo kwani ujenzi
unaoendelea katika soko hilo upo kinyume na sheria kutokana na halmashauri hiyo
kutangaza kwamba ifikapo Machi mosi mwaka huu wafanyabishara wa soko hilo wawe
wameshahamia katika masoko waliyopangiwa.
Nzingula alisema kutokana na
kampuni hiyo kukaidi agizo halali la serikali, hivyo halmashauri kupitia
wanasheria wake wanakamilisha taratibu za kuifikisha mahakamani kampuni
hiyo ili taratibu zingine zifuatwe.
Aidha Nzingula aliwataka
wafanyabishara kutoendelea kuwekeza katika soko hilo, na badala yake
waende katika masoko waliyoelekezwa na serikali kabla ya hatua zingine za
kuwaondoa hazijatumika.
Hata hivyo uongozi wa Soko hilo,
ulikiri kupokea barua ya kusitisha ujenzi huo na kusema kwamba huo si
ujenzi bali ni ukarabati wa mabanda ambayo yameanza kuchakaa baada ya
kudumu kwa muda mrefu.
Mmoja wa Viongozi Aley Shaban
alisema, baada ya kupoke abarua hiyo waliamua kusitisha ukarabati huo, huku
akisema soko hilo lipo kisheria kutokana na serikali kulitambua
tangu kuanzishwa kwake.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment