MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 23 February 2015

MSAADA KWA WATOTO YATIMA, MAUAJI YA ALBINO YALANIWA


Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Honorata Michael Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Honorata kilichopo Temeke jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Halima Ramadhan Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwadaliwa kilichopo Tegeta jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, ikiwa ni moja ya misaada inayotolewa katika vituo mbalimbali vya kulelea watoto yatima wakati wa msimu huu wa maadalizi ya Tamasha la Pasaka linalotimiza miaka 15 tangu lianzishwe.

Tamasha hilo Litafanyika jijini Dar es salaam Aprili 7 2015 na kushirikisha waimbaji mbalimbali wa kimataifa na waimbaji wa ndani, Katika Tamasha hilo pia kutakuwa na michezo mbalimbali itakayochezwa ikiwa ni pamoja na kukabidhi zawadi na vikombe kwa washiriki wa Tamasha hilo, Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo zilizoko Kinondoni jijini Dar es salaam.

Alex Msama amelaani mauaji ya Albino na kuiomba serikali kuweka mkazo katika kushughulikia wahalifu wanaofanya ukatili huu na kuua watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino), ili kukomesha mauaji hayo hapa nchini ambayo yanalitia aibu taifa(PICHA NA FULLSHANGWE).
Na Mwanaharakati.

No comments: