Katika uzinduzi huo, ulioudhuliwa na viongozi mbalimbali wa kisiasa,
kidini, ulinzi na usalama, mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongela, amesema
kuwa hakuna kinachoweza kuwa kimekamilika kwa asilimia mia moja, hivyo
kutokana na mtazamo na jinsi mwananchi atavyoielewa,ndivyo aelekeze kura
yake..........Mkuu huyo wa mkoa, amesema kuwa Biblia na Quran, watalaamu wanasema ingeandikwa kwa kufuata matukio yote ya Yesu na mtume Mohamad, mpaka leo ingekuwa haijakamilika, hivyo hata katiba hii pendekezwa ina mapungufu, ambayo yanaweza kuendelea kufanyiwa marekebisho kwani hata Marekani walishafanya marekebisho mengi japo katiba ni ya miaka zaidi ya 200. | | |
|
No comments:
Post a Comment