Bondia
mashuhuri wa kulipwa nchini, Francis Cheka, ambaye maarufu kwa jina la SMG
(pichani), amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya Sh, milioni
moja kwa kosa la kumpiga meneja wa baa yake, Bahati Kibanda.
Cheka alitiwa hatiani Julai 2 mwaka jana kwa kumpiga na kumsababishia maumivu makali Kibanda ambaye alikwenda hapo kudai fedha zake katika baa aliyokuwa anaifanyia kazi ijulikanayo kwa jina la Vijana Social Hall.
Hakimu Mwanamizi wa mahakama ya mkoa wa Morogoro Mhe. Said Msuya alikubaliana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na kuthibitisha shitaka hilo.
Hakimu Msuya alisema kuwa adhabu hiyo ni fundisho kwa mshitakiwa na watu wengine wanaotumia vibaya nguvu zao kwa watu wengine na anatakiwa kumlipa mlalamikaji fidia ya Sh milioni moja.
Pamoja na Cheka kupewa nafasi ya kujitetea, bondia huyo hakutoa maelezo yoyote na kuiachia mahakama hiyo kutoa adhabu inayostahili kwa bondia huyo aliyejizolea sifa kemkem katika ngumi za kulipwa nchini.
Hata hivyo, taarifa zilizotufikia wakati tunakwenda mitamboni, familia ya Cheka inasemekana ina mpango wa kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment