Katika taarifa iliyotolewa jana na uongozi wa Azam haikusema
sababu za klabu hiyo kumfungashia virago Omog ambaye katika miezi14
aliyokuwa Chamazi aliwasaidia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara
kwa mara ya kwanza.
Tetesi za kutaka kutimuliwa Omog zilianza baada ya
timu hiyo kutolewa katika robo fainali ya Kombe la Mapinduzi na Mtibwa
Sugar kwa penalti, lakini uongozi wa Azam ulikanusha taarifa hizo.............
Tangu wakati huo Azam imekuwa haina matokeo mazuri
katika Ligi Kuu ikiwemo kufungwa na Ndanda 1-0, JKT Ruvu (1-0) pamoja
na kutoka suruhu na Ruvu Shooting na Prisons na sasa ipo nafasi ya pili
ikiwa kwa pointi 27, wakati Yanga ikiongoza kwa pointi 31.
Hata hivyo, ndoto ya Azam kutaka kufanya vizuri
katika mashindano ya Afrika ilivunjika Jumamosi iliyopita baada ya
kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa El Merreikh hivyo kutolewa kwa
jumla ya mabao 3-2.
Mbali ya Omog, Azam pia imevunja mkataba na kocha wake msaidizi Ibrahim Shikanda aliyewahi kuwa mchezaji wa kikosi hicho.
Mabingwa hao sasa watakuwa chini ya kocha msaidizi
George Best Nsimbe wakati watakapoikabili JKT Ruvu Jumamosi ijayo
katika mechi ya ligi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Kutimuliwa kwa makocha hao ni mwendelezo wa timua timua ndani ya
Azam ambayo awali ilimfukuza kocha Neider dos Santos baada ya kufungwa
na ikawa chini ya Itamar Amorin.
Itamar aliondoka kwa sababu ya kuzidiwa nguvu na
wachezaji wasio na nidhamu mbele ya uongozi na timu akakabidhiwa kocha
Stewart Hall, lakini aliondolewa katika mazingira ambayo hayakueleweka
na akaajiriwa kocha Boris Bunjak kutoka Serbia.
Mserbia huyo hakudumu baada ya kufungwa na Simba
naye akafukuzwa na kurudishwa Stewart na akafanikiwa kuzifunga Simba na
Yanga katika msimu wa 2013/14, lakini haikutosha baada ya mzunguko wa
kwanza, akaambiwa aondoke. Timu hiyo ikakabidhiwa kwa Omog.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment