Kamati Kuu ya CCM imezidi
kuwaweka gizani makada sita waliomaliza adhabu ya kufungiwa kwa miezi 12
baada ya kueleza kuwa uchunguzi dhidi yao unaendelea kwa muda
usiojulikana, uamuzi utakaowazuia kujitokeza rasmi kutangaza nia ya
kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho tawala.
Edward Lowassa, Bernard Membe, Frederick Sumaye,
William Ngeleja, Stephen Wasira na January Makamba, ambao walipewa
adhabu hiyo Februari 18 mwaka jana, sasa watalazimika kusubiri hadi hapo
Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM itakapomaliza uchunguzi wake, ikiwa
imebaki miezi isiyopungua mitatu kabla ya wanachama kuanza harakati za
kuwania nafasi mbalimbali.
Kwa kawaida, CCM huruhusu wanachama wake kuanza
kuchukua fomu za kuwania urais.........
ubunge na udiwani kati ya mwezi Mei na Juni na kabla ya hapo huruhusiwa kutangaza nia ya kugombea nafasi wanazotaka, fursa ambayo makada hao wameikosa hadi sasa.
ubunge na udiwani kati ya mwezi Mei na Juni na kabla ya hapo huruhusiwa kutangaza nia ya kugombea nafasi wanazotaka, fursa ambayo makada hao wameikosa hadi sasa.
Katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, Nape
Nnauye aliwaambia waandishi wa habari jana baada ya kumalizika kwa kikao
cha Kamati Kuu, kuwa kwa kuzingatia kanuni za maadili ya CCM,
mwanachama aliyepewa onyo kali atakaa chini ya uangalizi kwa kipindi
kisichopungua miezi 12,
“Baada ya miezi hiyo kwisha, Kamati Ndogo ya
Maadili inaendelea na kazi yake kuchunguza mienendo yao hao waliokuwa
wamepewa adhabu katika kipindi chao cha adhabu cha miezi 12 kama
wametekelezaje masharti ya adhabu,” alisema Nnauye.
Alisema kazi ya kamati hiyo ndogo ni kuchunguza
ili kubaini kama makada wote sita walitimiza masharti ya adhabu
waliyopewa na kwamba itakapomaliza uchunguzi katika muda usiojulikana
itapeleka taarifa Kamati Kuu.
“Itachukua wiki, itachukua mwezi, itachukua miezi
ni kwamba itakapokamilika na Kamati Kuu kama kutakuwa na taarifa yoyote
tutautaarifu umma juu ya kinachoendelea,” alisema Nnauye.
Kikao cha Kamati Kuu, ambacho huhusisha viongozi
wa juu serikalini na kwenye chama hicho tawala pamoja na wanachama 14 wa
kuchaguliwa kutoka Zanzibar na Bara, kilifanyika Ikulu na Nape aliongea
na waandishi wa habari kwenye ofisi ya Umoja wa Vijana wa CCM iliyo
Lumumba.
Kati ya waliofungiwa, Wasira, ambaye ni Waziri wa Kilimo na Ushirika, ni mjumbe wa Kamati Kuu.
Lowassa, aliyekuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa
Serikali ya Awamu ya Nne, na Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, ndiyo wanaochuana vikali na wafuasi wao
wamekuwa wakishambuliana kwenye mitandao ya kijamii.
Sumaye pia alikuwa Waziri Mkuu kwenye Serikali ya
Awamu ya Tatu, wakati Ngeleja, ambaye amepewa adhabu kubwa zaidi
kutokana na kuhusika kwake kwenye sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow,
alikuwa Waziri wa Nishati na Madini, na Makamba ni Naibu Waziri wa
Sayansi na Teknolojia.
Makada hao ambao walipewa kifungo cha miezi 12
Februari 18 mwaka jana, baada ya chama hicho kubaini kuwa walianza
kupiga kampeni mapema kinyume na utaratibu wa CCM, bado hawajatangaza
nia ya kutaka kuwania urais mwaka huu ingawa habari zinasema kuwa
walishakusanya nguvu za kuanza mchakato huo baada ya kutoka kifungoni.
Habari zinasema kuwa makada hao walikuwa wanasubiri uamuzi wa Kamati Kuu
ili waingie rasmi kwenye kinyang’anyiro cha urais huku baadhi wakipanga
hafla kubwa za kutangaza nia.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment