Tume
ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia wananchi wote wa Mkoa wa Njombe,Halmashauri
ya Mji mdogo wa Makambako kuwa itaanza zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu
la Wapiga Kura kwa kutumia teknolojia ya “Biometric Voters Registration”
kuanzia tarehe 23/02/2015 hadi tarehe
01/03/2015 katika kata ya Kitisi, Kivavi, Lyamkena, Maguvani, Majengo,
Makambako, Mjimwema, Mlowa, na Mwembetogwa. Kata ya Kitandililo utafanyika
tarehe 03 -09/03/2015. Kata ya Mahongole tarehe ............
11-17/03/2015 na Kata ya
Utengule uboreshaji utafanyika tarehe 19 – 25/03/2015.
Vituo
vya Uandikishaji vitakuwa kwenye Vijiji, Vitongoji na Mitaa
Watakaohusika katika zoezi hili ni wananchi
wote:-
·
Waliotimiza umri
wa Miaka 18 na kuendelea
na wale wote watakaotimiza miaka
18 ifikapo mwezi Oktoba, 2015.
·
Waliojiandikisha
awali kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la zamani ili kuhuisha taarifa
zao na kupata kadi mpya za kupigia kura.
·
Wale wote ambao
wanazo sifa za kujiandikisha lakini
hawajawahi kujiandikisha kwenye Daftari.
Zoezi
litaanza kufanyika Mkoani Njombe katika Halmashauri ya Mji wa Makambako na Mji
wa Njombe.
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi inasisitiza wananchi wote wa Mji Mdogo wa Makambako kujitokeza kwa wingi kuanzia tarehe 23/2/2015 mpaka tarehe 25/03/2015
kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili kuwawezesha kupiga Kura
ya Maoni na kuchagua Viongozi wao katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2015.
Vituo
vya kujiandikisha vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 Asubuhi na kufungwa saa 12:00
jioni
Kumbuka:-
Hutaweza
kupiga Kura ya Maoni au Kupiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu kama utakuwa
hujajiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Nenda kajiandikishe sasa.
Ruth
Masham
Kny: Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment