Nicolaus Mac (None Association Movement) KWA MATANGAZO YA REDIO NA TV WASILIANA NASI KWA +255767814844- nicolausngaiza@gmail.com.
Sunday 8 March 2015
SIKU YA WANAWAKE DUNIANI; UKOSEFU WA AJIRA KWA AKINA MAMA WENGI MKOANI KAGERA WATAJWA KUWA NI UNYANYASAJI WA KIJINSIA.
Siku ya wanawake duniani, mkoani Kagera inasherehekewa huku wanawake wakiwa na kilio cha kutopata fursa ya kufanya kazi.
Katika kuelekea kilele cha siku hiyo Mach 8 2015, baadhi ya akina mama walioongea na sauti ya mnyonge, wamesema kuwa ujumbe wao mkuu mwaka huu ni mwanamke kuthaminiwa kupata ajira kwani wanaweza kufanya kazi na kuinua familia.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, akina mama wa umoja wa kamati za kina mama mkoani Kagera UWAKUTA, wamesema kuwa ...................
jamii ya mkoa wa Kagera imekuwa na fikra kuwa mwanamke hawezi kufanya kazi kwa ufasaha, huku akinyimwa uhuru wa kuongea katika jamii, hivyo kushindwa jinsi ya kujitetea.
Mwenyekiti wa umoja huo wenye wajumbe 18 kutoka halmashauri zote za mkoa wa Kagera, Bi Aneth Rushobe, ameomba serikali na wadau wa maendeleo, kuwapa kipaumbele cha ajira wanawake mkoani Kagera kwani wanaweza bila kuwezeshwa.
Amesema juhudi za umoja huo ni kuhakikisha wanatoa elimu kwa akina mama ili wawe na mwamko katika kuzisaka ajira, siyo tu serikalini bali hata katika sekta binafsi, huku akisema kuwa wadau pia wasaidie kubadili mfumo wa fikra finyu za baadhi ya wanaume mkoani humo kuwa wanawake hawawezi kununua matumizi ya nyumbani na kuongeza maendeleo ya jamii.
Kwa mujibu wa takwimu za sensa ya watu na makaazi 2012, mkoa wa Kagera una wanawake milioni moja laki mbili elfu hamsini na mbili na mia tatu arobaini (1,252,340) wenye umri kuanzia miaka 0 hadi 60, wenye uwezo wa kufanya kazi ni laki tano elfu therathini tisini na watano (5,300,95) lakini wanaofanya kazi ni elfu tano na mia tatu ishirini na watano (5,325)tu, huku kiwango kikubwa ambao ni laki tano elfu ishirini na nne na mia saba sabini ni mama wa nyumbani.
Wanawake mkoani Kagera, pamoja na kukosa ajira za kuajiriwa serikalini, pia hawana desturi ya kufanya kazi ngumu kama walivyo wanawake wa makabila mengine ya Kisukuma, Kikurya nk , mfano kuchimba mitaro, kugonga kokoto, kuendesha baiskeli kama usafiri wa kawaida, kuchanja kuni na hata hawana desturi ya kujishughulisha na kazi za ujenzi wa nyumba na miundombinu mingine kama hiyo, badala yake huchota maji katika familia, kumenya ndizi na kupika chakula.
Wanawake kuchagua kazi hizo laini, kumejenga desturi kwa jamii ya mkoa wa Kagera, kuwa mwanaume akifanya kazi za kike kama kupika,kuchota maji na kumenya ndizi basi anatambulika kama amerogwa na mwanamke.
Maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani, mkoani Kagera imeadhimishwa kwa akina mama kutembelea wakina mama na watoto waliolazwa katika hospitali ya mkoa wa Kagera, ambapo wametoa bidhaa zenye thamani ya shilingilakitatu na elfu hamsini, zikiwemo pea kumi za khanga, sabuni box nne, juisi box nne na mafuta ya kupaka.
Na Mwanaharakati.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment