Kamanda wa polisi Kagera Henry Mwaibambe, akionesha baadhi ya vifaa na silaha zilizokamatwa. |
Jeshi
la polisi mkoani Kagera linashikilia bunduki nne aina ya SMG pamoja na sare mbalimbali za jeshi la Burundi
.
Akiongea
na waandishi wa habari ofisini kwake, kamanda wa jeshi la polisi mkoani kagera
HENRY MWAIBAMBE, amesema kuwa...............
bunduki hizo zimekamatwa katika pori la Nyantakara lililopo katika halmashauri ya Biharamulo.
bunduki hizo zimekamatwa katika pori la Nyantakara lililopo katika halmashauri ya Biharamulo.
Mwaibambe
amesema kuwa katika kufanikisha kukamatwa kwa bunduki hizo, kumetokana na kupewa
taarifa na raia wema ambapo polisi liliweka mtego na kufanikisha kukamata kwa
bunduki hizo.
Aidha
katika tukio hilo hakuna jambazi aliyekamatwa ambapo limekamata magazine
sita pamoja na risasi 129.
Bwana
mwaibambe amesema kuwa katika tukio hilo lilitokea mapema Mach 13 , polisi ilijibizana
kwa risasi na majambazi hayo .
Hatahivyo
polisi mkoani Kagera inawashikilia watu 15 kwa tuhuma za matukio ya mauaji
yaliyojittokeza katika manispaa ya bukoba.
Akiongea
na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Kagera HENRY MWAIBAMBE amesema
kuwa watuhumiwa hao wanaendelea na mahojiano na ushaidi ukikamilika
watafikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji.
Kamanda
mwaibambe ameongeza kuwa katika kuwatafuta watuhumiwa wa mauaji hayo jeshi la
polisi limejipanga ambapo aamesema kuwa wale wote waiyohusika watatiwa mbaroni.
Aidha
kamanda mwaibambe amesema kuwa anaendelea kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano
kwa jeshi hlo ili kuwezesha jeshi hilo kufanikisha zoezi lao la kuutia mbaroni
mtandao mzima.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment