Jeshi la polisi mkoani rukwa
linawashikilia watu saba hadi sasa, kwa tuhuma za kuhusika na kitendo cha
kikatili cha kukata kiganja cha mkono wa kulia, cha mtoto mwenye ulemavu wa
ngozi Baraka Cosmas Lusambo mwenye umri wa miaka sita, katika kitongoji cha Kikonde
kata ya Kipeta wilaya ya Sumbawanga vijijini, ambapo pia katika tukio hilo
wamemjeruhi mtoto huyo mkono wa kushoto na mama yake kupigwa kichwani.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Rukwa kamishna msaidizi wa polisi Leons Rwegasira, amesema wamefanikiwa
kuwakamata watu hao kufuatia msako mkali, mara tu baada ya kutokea tukio hilo
kwenye kitongoji hicho cha Kikonde,..............
ambacho kinakuwa na wakazi wakati wa msimu
wa kilimo na kiangazi watu wanahama tena, katika familia yenye watoto wengine
watatu wenye ulemavu wa ngozi.
ACP.Rwegasira pia amesema kwenye
msako huo mkali, wamefanikiwa kuwakamata watu wanane wanaojihusisha na uganga
wa jadi na upigaji wa ramli chonganishi, ambacho ni chanzo kikubwa cha
kusababisha vifo na kujeruhiwa watu wenye ulemavu wa ngozi kwa imani za kishirikina.
Waganga hao wamekutwa na nyara za serikali, ikiwamongozi ya chui, nyayo za mbuni, nywele za binadamu na mifupa.
Mtoto baraka na mama yake mzazi
wamelazwa kwenye hospitali ya rufaa ya jijini mbeya, wakitibiwa majeraha
waliyoyapata wakati wa purukushani za kumshambuliwa mtoto huyo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment