Habari za kusikitisha kutoka kata ya
Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga ni kwamba watu zaidi ya 20 wanadaiwa
kufariki dunia baada ya kuangukiwa nyumba kutokana na mvua kubwa iliyonyesha
eneo hilo usiku wa kuamkia leo.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kuwa hadi sasa watu 24 wameopolewa baada ya nyumba zao kuanguka, huku zingine zikiingiwa na maji.............
Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kuwa hadi sasa watu 24 wameopolewa baada ya nyumba zao kuanguka, huku zingine zikiingiwa na maji.............
Hali hiyo inadaiwa kuleta majanga zaidi kutoka na nyumba zilizojengwa kwa udongo kuharibiwa vibaya na mvua hiyo.
Wakati huo huo wiki iliyopita WATU watano wa familia moja wakiwemo
wanafunzi wanne walipoteza maisha kwa kupigwa radi wakiwa shambani katika
Kijiji cha Manungu kata ya Uyogo, Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama, mkoani
Shinyanga.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
jana na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kahama, Leonard Nyadaho, kwa niaba ya
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, watu hao walipigwa na radi Februari 28,
mwaka huu na kufariki papo hapo kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.
Nyadaho alisema mvua hiyo iliyoanza
kunyesha juzi jioni katika kijiji cha Manungu kitongoji cha Izengwe. Alisema
mvua hiyo iliwakuta wananchi hao wakiwa mbugani wakipanda mpunga ndipo
walipopigwa na radi na kufariki.
Aliwataja marehemu hao kuwa ni Paulina
Williamu (28), Magreth Mayunga (13), Herena Mayunga (14), Flora Mathias (13) na
Veronica Mathias (14), wote wanafunzi wa Shule ya Msingi Manungu.
Mashuhuda walisema marehemu hao
waliamka asubuhi na kwenda shambani kupanda mpunga, wakiwa huko ghafla
lilitanda wingu zito ndipo mvua iliyoambatana na radi ilipoanza kunyesha.
Walisema mvua hiyo kubwa iliyokuwa
imeambatana na upepo mkali ilikuwa na muungurumo wa radi wa mara kwa mara.
Walisema ilinyesha muda mfupi na ilipokatika walisikia mayowe yakitokea
walipokuwa watu hao
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment