Mfumo wetu wa Bunge tulionao sasa hivi unaruhusu kila mtu
kuingia bungeni kufuata anachokitaka yeye, badala ya wanachokitaka
wananchi.
Mimi pamoja na watu wengine wanaofuatilia mambo ya
siasa hapa Tanzania, tumekuwa tukisubiri kwa hamu kujua jimbo la
uchaguzi atakalogombea Saida Karoli.
Hata kama siyo jimbo labda udiwani au ubunge wa
viti maalumu kupitia chama chochote cha siasa. Umaarufu aliojijengea
Saida Karoli, kwa siku za hivi karibuni unamtosha kabisa kuwa mwakilishi
wa Watanzania ndani ya Bunge au kwenye vikao vya halmashauri ya wilaya
na miji............
Saida ana sauti nzuri inayopendwa na watu wengi
hapa Tanzania, Afrika ya Mashariki na kwingineko duniani. Umaarufu wake,
kipato chake na kampuni yake, vinamtosha kuwa mgombea na kupita!
Wabaya wake wanasema amefulia, lakini bado yuko na
anaendelea na shughuli zake.
Haiwezi kutushangaza kumsikia akijitangaza kugombea ubunge. Siyo kwamba watu wanawataka wabunge na kuwaomba kugombea, bali wao wana nia ya kugombea!
Haiwezi kutushangaza kumsikia akijitangaza kugombea ubunge. Siyo kwamba watu wanawataka wabunge na kuwaomba kugombea, bali wao wana nia ya kugombea!
Katika hali ya kawaida, mtu huwezi kuomba
kuwatumikia watu, bali watu wanaweza kukuomba kuwatumikia! Ubunge au
udiwani ni uwakilishi, ni kuwasemea wengine; ni kutumwa na wengine. Ni
kibarua kigumu maana mtu anakuwa na wajibu wa kusema yale aliyotumwa na
wengine.
Ni kazi ngumu ambayo mtu anayeamua kuiomba anakuwa
na roho ngumu; vinginevyo ni kazi ambayo watu wenye uwezo (kisomo na
upevu wa fikra) katika jamii wanaombwa kujitolea kutumwa!
Siku za nyuma ili kuwa mwakilishi ilikuwa ni
lazima mtu atimize sifa. Ilikuwa ni lazima mtu awe mwanasiasa na
mzalendo wa kweli. Vilijengwa vyuo vya siasa na maadili! Pia kulikuwa na
miiko. Siyo kila mtu angeweza kujibatiza mwanasiasa na kutaka kuwa
mwakilishi.
Leo hii ni ‘utandawazi na siasa huria.’
Tumefunikwa na jinamizi na kujidanganya kwamba kila mtu anaweza kuwa
mwanasiasa! Na wengine wanakwenda mbali na kujiaminisha kwamba kila mtu
anaweza kuwa daktari au profesa. Tuna madaktari na maprofesa wengi,
lakini vitabu vichache! Hawa madaktari na maprofesa tunaowasikia
mitaani, waliandika nini na kutafiti nini inabaki kuwa kitendawili na
ndoto za mchana!
Inashangaza kwamba uchaguzi wa mwaka 2010; Jina la
Saida Karoli, halikujitokeza. Inashangaza kidogo maana wasanii wenzake
ambao anawapita kwa mbali majina yalijitokeza. Labda ni kwa vile
hajazunguka na kutumbuiza kwenye kampeni za CCM? Akipata maarifa ya
kufanya hivyo mwaka huu, ni lazima jina lake litajitokeza!
Wagombea wengi waliojitokeza kwenye uchaguzi wa
mwaka 2010 na hasa wale wa kupitia chama tawala, walitufumbua macho
kwamba siasa hapa Tanzania ni uwanja wa kila mtu. Hakuna sifa, elimu,
karama na uwezo wa kuchambua mambo mbalimbali katika jamii na dunia
nzima kwa jumla na wala siyo lazima mtu awe mwanasiasa! Sifa kuu ni
umaarufu na fedha.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment