MAMENEJA wa Tanesco kanda yaziwa
wametakiwa kutoa taarifa za mgao wa umeme kwa wateja kupitia vyombo vya habari
hasa Radio za kijamii ili kuchukua tahadhari ya kuharibikiwa mali zao
majumbani au taasisi husika.
Naibu waziri wa Nishati na madini Bw
Charles Mwijage amesema hayo wilayani Biharamulo wakati wa ziara yake ya
kukagua mitambo ya kufua umeme wilayani humo akiwa katika ziara ya kikazi
katika mikoa ya kanda ya ziwa.
Bw Mwijage amesema kuwa wananchi
wanapata hasara..........
zitokanazo na mgao wa umeme unaotokea bila wao kutaarifiwa na
kusababisha madhara makubwa kwenye vyombo na mali zao hivyo watumie radio
kuwafahamisha wateja kinachotokea.
Hata hivyo amesema mgao huo
unatokana na uchakavu wa mitambo ya kufua umeme ambapo baada ya
ukaguzi wataalamu wa wizara yake watafanya jitihada kuhakikisha mgao
unasitishwa ndani ya siku 45 katika mikoa ya kanda ya ziwa.
Wakati huo huo kule Ngara, serikali
imeahidi kumaliza tatizo la mgao wa umeme ndani ya siku 45 kwa wakazi wa
mji wa Ngara na maeneo jirani mkoani kagera baada ya kukamilisha ukarabati wa
mashine ya kufua umeme yenye uwezo wa kuzalisha megawati 400 mjini humo.
Naibu waziri wa nishati na madini Bw
Charles Mwijage amesema hayo hii leo baada ya kufanya ziara ya siku moja kukagua
mitambo ya kufua umeme katika eneo la Nakatunga na Djululigwa wilayani humo.
Bw Mwijage amesema kuwa Wilaya ya
Ngara ina mahitaji ya megawati 1200 za kutosheleza wananchi kupitia Tanesco
lakini kutokana na uchakavu wa mitambo kunakuwepo mgao ambao unachangia
wananchi kushindwa kuzalisha kiuchumi.
Hata hivyo amesema serikali inafanya
mchakato wa kuhakikisha wananchi wanatumia umeme wa gridi ya Taifa ikiwa ni
pamoja na ule utakaozalishwa katika maporomoko ya Rusumo na kusambazwa katika
nchi za Rwanda na Burundi.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment