MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday, 8 May 2015

BREAKING NEWS!!! RAIS KUMRUDISHA KATIBU MKUU NISHATI NA MADINI BAADA YA KUKOSA TUHUMA?

Katibu mkuu kiongozi wa jamuhuri ya muungano wa tanzania Balozi Ombeni Sefue ametoa taarifa hiyo baada kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi dhidi ya katibu mkuu huyo wa zamani Eliakim Maswi.

Uchunguzi uliofanywa kuhusu  tuhuma za Maswi  kuhusishwa na  sakata la TEGETA ESCROW, imebainika kuwa Maswi hana hatia na hajausika kwa namna yeyote kwenye kashifa hiyo.

Hatahivyo  ripoti hii dhidi ya Mawsi tutaikabidhi kwa Mh Rais kwa lengo kuwa aipitie tena maana yeye ndiye mwenye mamlaka ya uteuzi wake, na ndiye aliyeniagiza nimsimamishe kwa uchunguzi mwishoni mwakajana, hivyo ataangalia utaratibu mwingine.

 

Maswi aliyekuwa kitibu mkuu nishati na madini alisimamishwa na Balozi Sefue kuanzia  Jumanne, Desemba 23, 2014, kwa kutumia madaraka aliyonayo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.

Taarifa iliyotolewa wakati huo na Ofisi ya Balozi Sefue mjini Dar es Salaam ilisema kuwa amechukua hatua hiyo “Kwa mujibu wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Na. 8 ya mwaka 2002 (kama ilivyorekebishwa)”ambapo “Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.

Hatahivyo Balozi Sefue alimkaimisha ukatibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi C. Mwihava, hadi uchunguzi dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi ulipotakiwa kukamilika.
Taarifa hiyo ya Balozi Sefue pia ilikariri kauli ya Rais Kikwete katika hotuba yake kwa Taifa jana, Jumatatu, Desemba 22, 2014 ambako Rais alisema yafuatayo:-

“Kuhusu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kwa vile ni Mtumishi wa Umma, anatawaliwa na Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma, hivyo nimeshaelekeza Mamlaka kuchunguza tuhuma zake na hatimaye ikibainika ana makosa hatua za kinidhamu zitachukuliwa.”

 

Ndugu Maswi, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Ndugu Frederick Werema pamoja na Mawaziri wawili walituhumiwa wakati wa Kikao cha Bunge kilichopita kuhusiana na Akaunti ya Tegeta Escrow.

Na Mwanaharakati.

No comments: