MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday, 8 May 2015

MAREHEMU WAAGWA CONGO, SIRI YA MAJINA ASKARI WALIOUAWA, MAJERUHI WATAJA SARE ZA WAHUSIKA

.Miili ya aagwa na wenzao, kiongozi wa UN awataka kuongeza juudi
.Majeruhi waendelea na matibabu, wengine watatu hawajulikani walipo
.Idadi ya waliouawa mpaka sasa yaongezeka, kwa askari wa Tanzania kwenye nchi mbalimbali.
INGAWA jeshi  la ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), limekiri kupokea taarifa za askari wawili waliouawa Mei 5, mwaka huu na wengine 16 kujeruhiwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imekuwa ngumu kutaja majina ya askari waliouawa.

Kaimu Msemaji wa jeshi JWTZ Meja Joseph Masanja, alisema wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam.

Waliuawa na kikundi cha waasi wa Allied Democratic Forces (ADF), wakiwa wanatekeleza jukumu lao la ulinzi wa amani, ambao ni sehemu ya wapiganaji wa Kikosi Maalumu cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa (MONUSCO), walioko kazini nchini DRC.
Shambulizi hilo lilitokea DRC Mei 5 saa 12:30 jioni, ambapo askari hao walikuwa miongoni mwa 46 waliokuwa katika jukumu hilo.
Awali askari wetu hao walisafiri kwa ndege kutoka mji wa Abralose kuelekea katika mji wa Mavivi, baada ya kufika katika mji huo, msafara wao ulielekea katika mji wa Mayimayi kwa njia ya barabara wakitumia magari ya kijeshi.
Wakiwa njiani kuelekea katika mji wa Mayimayi, ndipo msafara wao ulipovamiwa na kikundi kinachodhaniwa kuwa cha waasi wa ADF na magari waliyokuwa wakisafiria yalishambuliwa kwa silaha za kivita, ambapo gari moja liliteketezwa na kusababisha vifo vya askari wawili papo hapo na wengine 16 kujeruhiwa.
Majeruhi hao walipelekwa hospitali kwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri. Kuhusu miili ya marehemu kurejeshwa nchini, alisema wanasubiri Umoja wa Mataifa (UN) kukamilisha taratibu zao kwanza.

Kiongozi wa UN kutembelea eneo la tukio.

Kiongozi huyo wa UN nchini DRC, Bw Martine Kobler ametoa pole kwa serikali ya Tanzania, na kuwasihi vijana waliobaki kuongeza nguvu na juhudi zaidi ya kutafuta amani DRC, japokuwa wanafanya kazi katika mazingira magumu mashariki mwa nchi hiyo.
Kwa upande wake gavana wa Beni  Julien Paluku wa Kivu kaskazini ametembelea eneo lililohusika na shambulizi huko Beni Kivu kaskazini.

Majeruhi katika tukio hilo, wamesema kuwa  walishambuliwa na askari walioonekana kuvaliasare za jeshi na kutambulika kama askari watiifu kwani walivaa sare za jeshi la serikali ya Congo, ambapo taarifa zisizorasmi kutoka jeshi hilo, nikwamba sare yake imechukuliwa na makundi mengi ya waasi na ni gumu kutambua nani muasi au mtiifu kwa wakati mmoja.
 
Kuagwa na makamanda wenzano;-
Miili ya askarihao imeagwa CONGO kwa taratibu zote za kijeshi tayari kupelekwa Tanzania kama inavyoonekana kwenye picha, huku umoja wa Mataifa umesema hauta kata tamaa kufatia mashambulizi ya waasi wa ADF



Matukio mengine kwa askari wa Tanzania.
Vifo vya wanajeshi hao wawili, kumefanya idadi ya wanajeshi wa Tanzania waliouawa miaka miwili iliyopita wakati wakilinda amani nchini DRC kufikia watano mpaka sasa.

Julai 2013 wanajeshi saba wa Tanzania waliokuwa wakilinda amani huko Sudan, waliuawa baada ya kushambuliwa na waasi, ambapo 17 walijeruhiwa vibaya.

Juzi ofisi ya UN nchini ilisema Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki-moon, amelaani mauaji ya wanajeshi hao, pia ametuma salamu za rambirambi kwa serikali na familia za wapiganaji hao mashujaa wa JWTZ.

Katika tukio hilo, wanajeshi wengine 13 wa DRC walijeruhiwa vibaya huku wanajeshi wengine wanne hawajulikani walipo. Tukio lilitokea mashariki mwa DRC, ambako majeshi ya Tanzania yapo kwenye vikosi vya Umoja wa Mataifa vya Kulinda amani.

Eneo hilo limekuwa likishambuliwa mara kwa mara na waasi wa DRC. Shambulio hilo limekuja zikiwa ni siku chache baada ya helikopta iliyokuwa na sehemu ya wanajeshi wa MONUSCO kushambuliwa kwa risasi na wapiganaji wa waasi kutoka eneo hilo.(PICHA NA AUSTERE MALIVIKA)
 

Na Mwanaharakati.

No comments: