MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday, 8 May 2015

MIGOMO NA MAFURIKO DAR KAGERA HALI SIYO SALAMA, WASIWASI WATANDA


.Kiwango ni milimita 8000 katika miaka mine.
.Uwapo wa waliojenga mabondeni na bila kufuata ramani.

Wakati wakaazi 6 jijini Dar es salaam wakipoteza maisha kutokana na mvua iliyonyesha katika kipindi cha siku tatu kati ya 4-7mei2015, mamlaka ya hali ya hewa nchini kupitia meneja wake mkoani Kagera Bw Silas Msoma, amesema kuwa mvua bado zinaendelea kunyesha mkoaniKagera na kunauwezekano wa kutokea mafuriko kwani zinanyesha chini na juu ya wastani.

Amesema takwimu zilizorekodiwa mkoani humo zinaonesha milimita 8,142.1 ya mvua kati ya 2011 na 2014 inaonesha kiwango cha milimita 2,030.1 kila mwaka,kiwango ambacho kinatakiwa kuchukua taadhali kubwa.

  

Mkurugenzi wa TMA Dr Agnes Kijazi, amezungumza leo kuhusu taadhari ya mvua na kusema kuwa itaendelea kunyesha hadi tarehe 20 Mei 2015, Bonyeza chini kumsikiliza. 
Hali tete Bukoba;-
Katika mfululizo wa miaka 4 tangu 2010, manispaa ya Bukoba imekuwa ikikumbwa na mfuriko katika maeneo kadhaa  ya mji huo,kama Omukigusha, Hamugembe, Omukizinga kata Bakoba, na baadhi ya maeneo yaliyozunguka mto Kanoni.
Katika maeneo  hayo, kumeshatolewa maelekezo na viongozi wa serikali ya mkoa na halmashauri kuwa wananchi waliojenga kwenye maeneo yanayopakana na mto Kanoni pamoja na mabondeni, kwani kila mwaka yamekuwa yakisababisha madhara ya nyumba kujaa maji na mali za wakaazi kuharibika.

Baadhi ya wakaazi waliozungumza na mtandao huu kwa masharti ya kutotajwa majina yao,wamesema kuwa hawawezi kuama kwasababu wameuziwa na serikali, ilhali wanalipia kodi ya nyumba pamoja na kuwa wana namba za utambulisho wa nyumba zao.
Wameomba serikalikuwafanyia utaratibu wa maeneo mbadala na fidia kwani walipitia taratibu zote stahiki, hadi kufikia kujenga kwa maelezo ya ofisi ya mipango miji.

Mafuriko jijini Dar es salaam;-
(MWANANCHI) Hali ya jiji la Dar es Salaam jana ilizidi kuwa mbaya kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kuwaweka wakazi kwenye hali ngumu zaidi baada ya kukumbwa na matukio mengine makubwa yaliyoathiri jiji na sehemu nyingine kote nchini tangu kuanza kwa mwaka.
Mvua hizo kubwa zinazolingana na zile................
zilizonyesha miaka mitatu iliyopita na kusababisha usumbufu mkubwa, jana zilisababisha nyumba kadhaa kuanguka, madaraja kukatika, barabara kufungwa, ikiwapo ya Morogoro, usafiri kuwa mgumu kutokana na misururu mirefu ya magari na Jeshi la Polisi kulazimika kutoa tamko la kushauri wananchi kutoka mapema maofisini ili kuwahi majumbani.

Matukio hayo yametokea siku chache baada ya kusitishwa kwa mgomo wa pili wa madereva uliosababisha usumbufu mkubwa kwa wasafiri karibu nchi nzima. Madereva waliamua kufanya mgomo huo kupinga masharti mapya ya kupata leseni yaliyotolewa na Serikali ikiwa ni mkakati uliobuniwa kukabiliana na ajali ambazo tangu Januari mwaka huu zimeua zaidi ya watu 900.

Mwaka 2015 pia umeanza kwa mgomo wa nchi nzima wa wafanyabiashara, kuibuka upya kwa mauaji ya albino, tishio la ugaidi lililoambatana na mauaji ya polisi na kugundulika kwa vituo vya mafunzo ya kigaidi kwa watoto wadogo, kuporomoka kwa kasi kwa thamani ya shilingi, kuvurugika kwa mchakato wa katiba na mvua ya mawe iliyoua watu kadhaa mkoani Shinyanga.

Kwa muda wa siku mbili, mvua zimenyesha mfululizo na kusababisha mafuriko kwenye sehemu kadhaa za Jiji la Dar es Salaam, ambalo ni kitovu cha biashara na shughuli za Serikali, likiwa na takriban watu milioni 4.4 kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.

Pamoja na mvua hizo kunyesha kwa wingi jijini Dar es Salaam, athari zake zinategemewa kugusa mikoa mingine yote kutokana na umuhimu wa jiji kiuchumi.

Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema jana kuwa daraja la Mwanamtoti lililopo eneo la Mbagala Kuu limeng’olewa na mafuriko hayo.

Kamanda Kova alisema Barabara ya Morogoro imefungwa eneo la kati ya Magomeni na Fire kutokana na Mto Msimbazi kufurika na kusababisha maji kupita juu ya daraja.
Alisema nyumba za watu wanaoishi Magomeni Mikumi zimejaa maji na hivyo Jeshi la Polisi limetoa amri kwa watu wote kuondoka eneo hilo.

Kova alisema barabara nyingine iliyofungwa ni ya Kinyerezi ambako maji yalikuwa yakiongezeka na kutishia kulisomba daraja linalounganisha Kinyerezi na Majumba Sita.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Temeke, Andrew Satta alisema daraja lililopo eneo la Mwanamtoti eneo la Mbagala Kuu limeng’olewa na mafuriko na kusababisha kukatika kwa mawasiliano.

“Nimewaagiza vijana wangu watembelee sehemu mbalimbali ili kuangalia maeneo ambayo yameathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam,” alisema Satta.


Na Mwanaharakati.

No comments: