MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 25 May 2015

MELI BUKOBA- MWANZA KUANZA SAFARI, PURUKUSHANI ZATISHA BANDARINI

. Ni Mv Serengeti ikiwa na uwezo mkubwa kuliko Victoria,
. Mazao yapanda bei ghafla,
. Nauli na gharama ya mzigo ni kama Victoria.
Mtandao huu umetembelea bandari ya Bukoba, na kujionea pilika za hapa na pale kukusanya na kupakia mizigo, huku wengine wakikata tiketi kwa ajili ya safari kuanza saa 12;00 jioni, na kutarajia kufika saa 12;00 asubuhi yake, kama alivyoeleza , kama msimamizi mkuu wa huduma za meli Bukoba, Mathew Mathias alivyozungumza nasi.

Pamoja na kuendelea kuonesha wasiwasi wao, baadhi ya abiria na hasa wasafirishaji wa mizigo, wameomba mamlaka kuboresha miundombinu hiyo, huku wakilalamikia ushuru unaopandioshwa mara kwa mara hasa wakati huduma hizi zimesimama.


Mv Serengeti, ilianza kazi katika ziwa Victoria mwaka 1988, ikiwa na uwezo wa kubeba mizigo tani 350, na abiria 593, ikitofautiana na Mv Victoria, iliyoanza kazi mwaka 1960, ikiwa na uwezo wa kubeba tani 200 za mizigo na abiria 1200.


Serengeti iliafuatia Mv Butiama iliyoanza kazi mwaka 1980 ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 100 za mizigo, huku meli iliyoitangulia Vctoria kule ziwa Tanganyika ya Mv Liemba 1913 na bado inafanya kazi, ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 200 za mizigo, Mv Clarias ilifuatia baada ya Victoria, tangu mwaka 1961, kwakuwa na uwezo wa kubeba abiria 293 na tani 10 za mizigo.

Taarifa za Mv Victoria, ni kwamba meli hiyo bado ipo kwenye matengenezo na wakatio wowote yaweza kukamilika na kuanza safari zake kawaida kutoka Bukoba kwenda Mwanza, kati ya saa 3;00 usiku hadi saa 12;00 asubuhi tofauti na Serengeti inayoanza safari saa 12;00 jioni hadi saa 12;00 asubuhi, na gharama ni zile zile hasa sehemu ya kukaa second seat sh 16,000 kwa kulala 26,000/= japokuwa Serengeti kuna vyumba vitatu tu vya kulala.

Na Mwanaharakati.

No comments: