MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday, 14 May 2015

TAARIFA ZA SASA KUHUSU BURUNDI

Kumekuwa na mapigano usiku kucha katika mji mkuu wa Burundi ambako kulikuwa na jaribio la mapinduzi ya kutaka kumng’oa madarakani rais, Pierre Nkurunziza. Rais huyo ameshindwa kurejea nchini mwake kutoka katika mkutano wa viongozi wa kanda,baada ya ndege yake kugeuza kurejea ilikotokea.

 Ingawa askari watiifu kwa rais huyo wamedai kuzima jaribio hilo la mapinduzi yaliyokuwa yakiongozwa na meja jenerali Godefroid Niyombare dhidi ya rais wao,na kwamba udhibiti wan chi uko mikononi mwao na hasa katika maeneo muhimu ya mji mkuu wan chi hiyo ,Bujumbura. Makabiliano ya risasi yamesikika karibu na vituo vya redio na runinga .mwandishi wa BBC aliyeko nchini Burundi amesema kwamba ameshuhudia jeshi likiwa limegawanyika pande mbili ,na haijulikani nani ameshikilia udhibiti wa nchi kwa sasa. 

 Rais Nkurunziza amekosolewa kwa haja yake ya kuwania muhula wa tatu wa uongozi nchini Burundi ,maamuzi ambayo yalisababisha wiki kadhaa za maandamano ambapo watu ishirini wameripotiwa kupoteza maisha. Maelfu ya watu wamekuwa katika shamra shamra katika mji mkuu wan chi hiyo Bujumbura baada ya wiki kadhaa za maandamano kumpinga katika maamuzi yake ya kugombea muhula wa tatu wa uongozi,na tayari mpaka sasa viongozi wakuu wa kanda wamelaani mapinduzi hayo. 

Mgogoro wa Burundi umezusha wasi wasi wa kurejea katika ghasia baada ya miaka kumi na miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Zaidi ya watu elfu tatu walikufa katika vita vya kikabila kati ya wahutu na watutsi ,vita vilivyomalizwa muongo uliopita.na mgogoro wa sasa nchini humo umehusisha kwa kiasi kikubwa na masuala ya kisiasa. lakini,yaliyojiri Burundi hayana tofauti na kilichojiri katika nchi jirani ya Rwanda ambayo ilikumbwa na mauaji ya kimbari nayo ilikabiliwa na masuala ya ukabila. 

Umoja wa mataifa umeonya hivi karibuni kwamba ikiwa ghasia zitasitishwa Burundi itakuwa na Amani na kama itakuwa vinginevyo basi nchi hiyo itarejea katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. CREDIT BBC
Na Mwanaharakati.

No comments: