. Wahapishwa kuthibitisha kujivua vyama
vyao,
. NEC yasisitiza kusimamia sheria hiyo,
. Mgeni rasmiaeleza umuhimu wawapiga
kura.
Uzinduzi wa semina hiyo umefanyika kwatika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kagera, na mgeni akiwa ni mkuu wawilaya Bukoba Jackson Msome, kwa niaba ya mkuu wa mkoa, kwa kuwasisitiza wanasiasa kutowaingiliawataalamuwakatiwa uandikishaji, na kusemakuwa ni dhaili kuwa wapiga kura ni muhimu lakini hawawezi kupatikana bila kuandikishwa, hivyo wahusika wahamasishe ipasavyo ili wajiandikishe wakutosha.
Viongozi hao kutoka ngazi ya halmashauri za mkoa wa Kagera
za Bukoba, Muleba, Misenyi, Karagwe, Kyerwa, Biharamulo,na Ngara, wamehapishwa
chini ya mwanasheria wa mahakama ya hakimu mkazi mkoani Kagera.

Mwandikishaji maafisa uandikishaji wasaidizi na maofisa
uchaguzi na waratibu wa uandikishaji wa mkoa wa Kagera, wameanza semina ya siku
mbili mkoani humo, ili tarehe ya uandikishaji mkoani humo ikitangazwa waweze kutimiza wajibu wao.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), juzi imetoa ratiba ya kuanza uandikishaji kwa kutumia mfumo wa BVR katika mikoa ya Mbeya, Rukwa, Katavi na Dodoma.
Kwa mujibu wa Tume hiyo, uandikishi litaanza siku ya ijumaa tarehe 15/05/2015 hadi siku ya jumapili kwa mikoa ya Mbeya, Katavi Rukwa na Dodoma. Uandikishaji utafanyika katika vituo vilvyoko katika vitongoji, mitaa na vijiji pamoja na kata zote za mikoa hiyo.
Aidha, vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2.00 asubuhi na kufungwa saa 12 jioni, ambapo Uboresshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura utahusisha, wapiga wote upya ambao ni raia wa Tanzania kuanzia umri wa miaka 18, wenye kadi ya zamani watatakiwa kuirudisha kituoni.
Mwananchi atachukuliwa alama ya vidole vyote kumi vya mikono na kupigwa picha kisha atapewa kadi yake hapo hapo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment