MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday, 12 May 2015

VIDEO; MPANGO WA TIKA ULIOZINDULIWA KATIKA MANISPAA YA BUKOBA, MIFUKO YA HUDUMA YALALAMIKIWA

. Mwananchi kuchangia elfu 10 anatibiwa mwaka mzima,
. Wakabiliwa na changamoto ya watu kutokubali kujiunga,
. Dawa zaadimika ilhali wananchi wapo kwenye mchango.
Ni mpango wa tiba kwa kadi ambao umezinduliwa katika manispaa ya Bukoba, kwa lengo la kusaidia jamii kupata tiba kirahisi na kwa gharamanafuu, pale ambapo mwananchi atalipia elfu 10 kwa mwaka na kupata huduma za tiba bila kujali ni za gharama kiasi gani.
Mtandao huu umezungumza na mkurugenzi wa sera mipango ya afya katika ofisi ya katibu mkuu wizara ya afya Bi Mariam Ally, muda mfupi baada ya uzinduzi huo.




Mradi huo umezinduliwa  kukiwa na malalamiko ya wananchi kuhusu utaratibu wanaokutana nao katika vituo na hospitali mbalimbali mkoani Kagera, na hasa kwa wazee na wasiojiweza, ilhali wengine wakisema kuwa wanakuwa wakikatwa pesa nyingi kwa matangazo ya kupata huduma huku wakienda kuzifuata wanaambiwa hakuna dawa.


Mkurugenzi wa mfuko wa bima ya afya nchini Bwana Eugene Mikongoti, amezungumzia changamoto hizo, na jinsi walivyojipanga kujitofautisha na mifuko mingine katika usimamizi na utoaji huduma kwa jamii.

Muundo wa huduma ya tiba kwa kadi TIKA, Unaanza na ngazi ya halmashauri, kwa kuwa na bodi za afya ya halmashauri,  Ngazi ya kata, kamati ya afya ya kata na Ngazi ya vituo yenye kamati ya usimamizi wa kituo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo mkuu wa wilaya ya Bukoba Jackson Msome





Hifadhi ya Jamii ni haki ya kila Mtanzania. Haki hii imeanishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 11(1) na Sera ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2003. haki hii pia.............
imeinishwa kwenye mkataba wa Kimataifa wa Haki za Binadamu wa mwaka 1948 pamoja na mikataba ya Shirika la Kazi Duniani(ILO).

Kwa mujibu wa Ibara ya 22 ya Azimio la Umoja wa Mataifa juu ya Haki za Binadamu la Desemba 10,1948, Kila raia, anayo haki ya Hifadhi ya Jamii. Hivyo Taifa lina wajibu wa kuhakikisha kuwa kiwango cha chini cha maisha kwa wananchi kinafikiwa kwa kuhakikishiwa usalama waupatikanaji kwa masuala yote ya msingi pindi dharura zinapotokea. Hii ni pamoja na masuala yote ya msingi ya kijamii bila kujali hali ya kipato namichango yao au ajira. Hatahivyo, uduni wa taarifa juu ya Hifadhi ya Jamii nchini Tanzania huminya fursa ya kutambua kuwa suala la Hifadhi ya Jamii ni suala la haki za binadamu.

Katika Tanzania, haki ya Hifadhi ya Jamii kwa wananchi wote imeainishwa kwa kuwekwa wazi katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1977,kama ilivyorekebishwa mwaka 1984, 1995 na 1998. Haki ya kwanza inajumuisha“Haki ya ustawi wa jamii wakati wa uzee, ugonjwa, ulemavu au kuacha kazi.
Nchini Tanzania,Mfumo wa Hifadhi ya Jamii unafuata nguzo tatu (3pillars) kamailivyo kwenye Sera ya Hifadhi ya Jamii (2003) Nguzo ya kwanza Hifadhi ya Jamii kwa wote ambayo hulipwa kwa kutumia kodi Nguzo ya pili; mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya msingi (mandatory schemes).
Nguzo ya tatu; Mifuko ya Hiyari (supplementary schemes)

Na Mwanaharakati.

No comments: