MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday, 12 May 2015

MRADI WA MAJI BUKOBA; WANANCHI TUNAUPENDA LAKINI MIUNDOMBINU YA BARABARA IMEKUWA KERO.


. Kurejeshwa miundombinu kwalalamikiwa kuchelewa,
. Buwasa yaomba ukamilike uwanusuru,
. Mkandarasi aomba muda zaidi.

Benki ya maendeleo ya Ufaransa kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania,  ilianza ujenzi wa mradiwa maji katika manispaa ya Bukoba, kwa lengo la kuonda tatizo la uhitaji wa maji ya lita milioni 14 kwa siku.

Pamoja na ujenzi wa mradi huo,ambao ulianza mwezi  juni 2013, kumekuwa na adha kwa wakaazi wa manispaa hiyo, kutokana na ubomoaji wa miundombinu ya barabara, na maeneo ya kuingilia majumbani pamoja na maeneo ya biashara, na kulalamikiwa na wananchi kwani miundombinu hiyo hairudishwi katika hali yake ya awali.
Hatahivyo,barabara kuu zinazoingia na kutoka katikati ya mji wa Bukoba ambazo ziko chini ya mamlaka ya barabara TANRDOADS, zimebomolewa na kushindwa kurudishiwa kuhofia kuleta madhara kama Rwamishenye na eneo la Rugambwa, kama alivyoieleza sautiyamnyonge, meneja wa TANROADS Kagera, mhandisi John Kalupare.
Miongoni mwa majengo yaliyokumbwa na adha hiyo ni pamoja na ofisi za serikali kama kituo kikuu cha polisi Bukoba, na hotel binafsi ya Victorious Petch
Muhandisi mshauri Bwana Fortunatus Kasimbi amesema kuwa mradi utakamilika baada ya miezi mine kutoka sasa,kwani ulitakiwa kukamilika tarehe tano april 2015, ambavyo wamepeleka pendekezo na ukarabati wa maeneo yaliyobomolewa itabidi yarudishiwe baada ya kupandisha maji kwa majaribio na kujiridhisha kuwa hakuna mivujo.
Mradi huu unagharimu shilingi bilioni 31 za kitanzania, zilizodhaminiwa na benki ya maendeleo ya Ufaransa kwa kushirkiana na serikali ya Tanzania.
Maitaji ya maji katika mji wa Bukoba ni lita milioni 14 kwa siku, ambapo kiasi kinachozalishwa kwasasa ni lita milioni 8 pekee kutokana na uwapo wa mvua, nah ii inasaidiwa na uwapo wa vyanzo kama ziwa Victoria yenye kutoa lita milioni 4 kwa siku, mto Kagemu na vingine vine vya maji bubujiko vya Nyakanyasi, Jermany Galary, Kisindi na cha mafumbo.

BUWASA ambayoni mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Bukoba, inamiundombinu ya kilomita 83 ambazo zipo kwenye mtandao kwenye kata 12 kati ya 14 za manispaa ya Bukoba, ambazo ni Kashai, Bilele, Bakoba, Miembeni, Ijuganyondo, Kibeta, Kitendaguro, Rwamishenye na kata ambazo zinafikiwa baadhi ya maeneo ni Kahororo na Kagondo.

Ujenzi wa mradi huu tunategemea usaidie kilomita 68 na utafikia kata ambazo hatufiki kwa sasa.

Hatahivyo mradi huu ulitegemewa kukamilika na kukabidhiwa katika miezi 18, tangu ulipoanza juni 2012, lakini mpaka sasa haujakamilika, na umekuwa ukiongezewa muda mara kwa mara bila taarifa kwa wananchi ambao wanaendelea kutatizika na ubovu wa miundombinu, huku mhandisi mshauri Bw. Fortunatus Kasimbi akisema kuwa wameomba miezi3 wamalizie,kwasababu wamefikia asilimia 80 za ujenzi kwa sasa
Mradi huo unaojengwa na kampuni ya Technofab Gammorn Toddy Joint Venture kutoka India, unahusisha ujenzi wa mabomba yenye urefu wa kilomita 65, ikiwemo ujenzi wa chanzo kipya cha maji eneo la Bunena, ujenzi wa mtambo wa kuchuja maji, ujenzi wa matanki mawili ya maji na ujenzi wa miundombinu ya kutibu maji.
Taarifa iliyopo kwenye tovuti ya mkoa wa Kagera, mkoa huo unatekeleza shughuli ya utoaji wa huduma ya maji kwa kuzingatia Sera ya taifa ya maji ya mwaka 2002,  Sheria ya maji na usafi wa mazingira Na.12 ya mwaka 2009,  Sheria ya utunzaji wa rasilimali za maji Na. 11 ya mwaka 2009,  MKUKUTA II,  Mpango wa maendeleo ya Millenia, na Dira ya Taifa inayoishia mwaka 2025.
Mambo yote hayo yamezingatiwa wakati wa kuandaa Programu kabambe ya maji iliyoanza kutekelezwa mwaka wa fedha 2006/07 na itakamilika mwaka 2024/2025
Tangu mwaka 1961 Mkoa wa Kagera umekuwa ukitekeleza miradi mbalimbali ya maji katika ngazi ya vijiji na miji, ambapo hadi kufikia mwaka 2014 hali ya huduma ya maji ni kama ifuatavyo:-
•  Wananchi wapatao 1,425,653 sawa na asilimia 58 waishio vijijini wanapata huduma ya maji safi na salama.
•  Asilimia 76 ya wakazi waishio katika Manispaa ya Bukoba wanapata maji safi na salama
•  Asilimia 69 ya wakazi wanaoishi katika miji midogo na miji mikuu ya Wilaya wanapata pia huduma hiyo.
•  Miradi mingi ya maji inaendeshwa na vyombo huru vya watumiaji maji (COWSOs) katika ngazi ya vijiji, ambapo jumla ya vyombo 215 vilikuwa vimeundwa hadi kufikia june 2014 vyenye jumla ya Tsh. 115,957,658.00 kwenye akaunti zao kwa ajili ya kugharamia uendeshaji wa miradai ya maji.
•  Halmashauri za wilaya zimeunda sheria ndogo za kulinda uharibifu wa vyanzo vya maji na mazingira.
•  Sheira mpya ya maji na usafi wa mazingira imewezesha uundaji wa vyombo huru vya watumiaji maji, ambapo jumla ya vyombo 215 vimeundwa na vingine viko kwenye hatua mbalimbali ya kutambuliwa, kuelimishwa na kusajiriwa.
•  Kila Halmashauri ina msajiri wa vyombo huru vya watumiaji maji.
CREDIT-SAUTIYAMNYONGE 

Na Mwanaharakati.

No comments: