Mkuu wa mkoa wa Kagera amewataka watendaji katika manispaa
ya ukoba, kuacha desturi ya kurudia masuala ambayo yameshapita kwa kushindwa
kutekeleza kazi ya wananchi.
Mongela, amesema hayo katika kikao cha baraza la madiwani
manispaa ya Bukoba, kwa kusisitiza kuwa huu ni wakati wa kazi na kila
linalofanyika litazamwe kwa maslahi ya watu wa manispaa siyo kwa masilahi ya
kiongozi yoyote.
Amemtaka mkurugenzi mpya wa manispaa hiyo, Bwana Aron
Kagurumjuli, kurudisha na kusimamia sheria na taratibu za nchi
Ameongeza kuwa yaliyopita yamepita na hakuna kulinda maslahi ya mtu kwani viongozi
wamekuwa na makundi ya kuanza kujadili baadhi ya viongozi, kuwa hiyo ndiyo
inachangia kuwagawa wananchi na hatimaye kuonesha mkwamo katika manispaa.
Baraza la madiwani wa manispaa, limekaa na kujadili
taarifa ya utekelezaji kutoka kila kata za manispaa, katika
kipindi cha januari hadi macjhi 2015, ukiwa ni mwendelezo wa vikao vyake, chini ya Naibu meya Alexander Ngalinda, Aliyekuwa meya na kuenguliwa kwa tuhuma mbalimbali kuhusu ukiukwaji baadhi ya taratibu za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, anendelea na kesi mahakamani, akiiomba mahakama kumwamrisha mkurugenzi wa manispaa kumfungulia ofisi aliyoondolewa tangu mwaka jana.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment