Uandikishaji huo umeanza katika manispaa ya Bukoba,
ambapo mtandao huu umetembelea vituo vya mtaa wa Pwani na Nyamkazi kata
Miembeni, uswahilini kituo na machinjioni kata Bilele, na kujionea uandikishaji
ukienda pole pole, jambo ambalo baadhi ya wananchi wamesema kuwa kama
wanaandikisha namna hii yawezekana wananchi wengi wakakosa fursa ya
kujiandikisha.
Lewis Josiah, ni mmoja kati ya wananchi waliopo
kwenye foleni ya uswahilini, na Bwana Mapula katika kituo cha Nyamkazi
wameeleza suala la kusuasua kwa uandikishaji.
Mmoja kati ya wakala kupitia chama cha mapinduzi Hud
Idd Miiruko, amesema kuwa wao wanaridhika na uandikishaji, ingawaje wanaenda
taratibu sana lakini watamaliza bila matatizo, naye mratibu msaidizi wa uandikishaji manispaa ya Bukoba Bw Abdon Kahwa, amefafanua hali hiyo
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeanza uboreshaji
wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura kwa kutumia mfumo wa kielektroniki wa (Biometric Voters Registration BVR) mkoani Kagera katika Manispaa ya Bukoba leo 21/05/2015 kuanzia asubuhi saa mbili,
ingawaje baadhi ya vituo kama Machinjioni uandikishaji umeanza saa3 baada ya
mashine kuchelewa kufikishwa.
Kulingana na ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) uandikishaji wa wananchi katika mkoa wa Kagera utafanyika kwa siku 29
kuanzia hiyo kesho Mei 21, 2015 hadi Juni 18, 2018 ambapo maoteo ya
uandikishaji ni wananchi 1,217,388 kwa mkoa wa mzima.
Wananchi wanaotarajiwa katika Halmashauri hizo ni
92,000 Bukoba Manispaa, Bukoba 148,033, Biharamulo 150,000, Karagwe 130,000,
Kyerwa 150,000, Missenyi 144,600, Muleba
198,600 na Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ni 128,000.
Aidha vituo vya uanduikishaji vilivyoainishwa katika
mkoa mzima wa Kagera nia 1,676 ambapo Bukoba Manispaa ni vituo 75, Halmashauri
ya Bukoa 250, Biharamulo 140, Karagwe
217, Kyerwa 207, Missenyi 174, Muleba 395,
na Halmashauri ya Wilaya ya Ngara 218.
Wananchi wa mkoa wa Kagera wote wanaokidhi vigezo
pia wenye umri wa miaka 18 wanahamasishwa kujitokeza katika vituo vitakavyokuwa
katika maeneo yao kujiandikisha ili waweze kupata haki ya kupiga kura katika
uchaguzi mkuu ujao mwezi Oktoba mwaka huu.
Taarifa ambazo mtandao huu bado unafuatilia, watoto kadhaa wamekamatwa huko Karagwe wakiwa kwenye foleni na haijajulikana kama ni raia wa Tanzania.Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment