
Amesema kuwa hospitali hiyo inakabiliwa na matatizo ya baadhi ya vifaa kutofanya kazi, kutokana na tatizo la umeme lililojitokeza katika eneo la chini la jengo hilo, ambalo lina ghorofa moja, hatahivyo hospitali hiyo ya wilaya, imetajwa kuwa na ukosefu wa mtego wa radi.
Wakati huo huo, kata ya kashai imetajwa kusumbuliwa na
magonjwa ya aina kumi, ambayo yamethibitika kuongoza katika kipindi cha januari
hadi machi mwaka huu.
Kwa upande wake diwani wa kata Kibeta, mchungaji Israel Mlaki, amesema kuwa wananchi walichanga na kununua kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa zahanati lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea, na kata Kagondo wananchi wameshauriwa kukatwa miti katika shule ya Kiteyagwa, ili kupunguza uhalifu wa watu kukabwa nyakati za usiku, ikilinganishwa na mauaji yanayoripotiwa katika manispaa ya Bukoba.
Mkurugenzi wa manispaa hiyo Bw Kagurumjuli Aron Titus,
amesema kuwa hawezi kuzungumzia kitu chochote wakati huu, kwasababu bado
makabidhiano ya ofisi yanaendelea, na akishakabidhiwa atalifanyia kazi na
kuelewa masuala mengine yanayozungumziwa katika manispaa hiyo.

Kikao cha kawaida cha madiwani wa manispaa ya Bukoba, kimepokea taarifa
mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za maendeleo kutoka kwenye kata 14,
katika kipindi cha januari hadi machi 2015, leo kitaudhuriwa na mkuu wa mkoa
wakati wa majadiliano.

Mwaka 2013, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kagera, mh. Fabiana Massawe, alizindua hospitali hiyo ya wilaya, kwa lengo la kuanza kutoa huduma za matibabu, lakini imekuwa ikikabiliwa na matatizo mbalimbali, kama alivyotaja diwani wa kata Nshambya,ingawa ni msaada mkubwa kwa wananchi katika manispaa ya Bukoba.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment