. Ameacha mjane na watoto 3
Alifikwa na umauti wiki hii
nyumbani kwake mkoani Mbeya, baada ya kulazwa jumanne alipochomwa na mwiba
katika shughuli zake za kijamii, na mguu kuvimba kwasababu alikuwa akisumbuliwa
na ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu, siku moja baadaye alipelekwa hospitali
mjini Mbeya na alipochunguzwa na mganga ilibainika ameshachelewa kupata tiba ya
mguu huo kwani sumu ilikuwa imeshaeneo mwili mzima.
Amezikwa kitongojini kwao Kaato, kijijini
Katangalala, kata Kaagya tarafa Bugabo, akiacha mjane Rehema Mwogofi na watoto
watatu, wakike mmoja mkubwa na wakiume wawili wanaokadiriwa kuwa na umri wa
miaka kati 4 na 7. 


Marehemu Freddy Bakalemwa, alizaliwa tarehe 2 may 1964 Bukoba vijijini, alifariki tarehe 13 may 2015 na kuzikwa tarehe 17 may 2015. Roho yake Mungu aiweke mahala anapostaili Amina.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment