. Kuchelewa kufikishwa mashine kwenye kituo,
. Waandikishaji walalamikia mafuta kwenye vidole vya wananchi,
. Waomba idadi ya wandikishaji kuongezwa.
Mwandishi wa mtandao huu ametembelea vituo 5 katika manispaa ya Bukoba, na kubaini matatizo ya uandikishaji hasa malalamiko ya wananchi wanaosema kuwa kwenye foleni kwa muda mrefu, wengine wakisema kuwa zaidi ya dk 25 zinatumika.
Mimi ni Lenatus Tegamaisho sikuandikishwa tangu jana hivyo niliacha nimejaza fomu na kuondoka ili nije kumalizia leo upigaji wa picha kama walivyonielekeza, na tulikuwa watu wengi hivyo walielemewa kutokana na sped ndogo.
Kwakweli wanatakiwa kuongeza watu zaidi anglau kila kitengo kiwe na watu wawili, kwasababu malalamiko yetu ya jana leo wameongeza mashine nyngine lakini speed ni ile ile kwasababu wanaozitmia hawakuongezeka.
Mtandao huu umezungumza na mmoja kati ya BVR Operator katika kituo cha Kahororo ofisi ya kata Justine Peter Bakera, na kusema kuwa wanashindwa kuwa na kasi ya uandikishaji kutokana na mashine kukwama baada ya watu wengine kuwa na mafuta kwenye vidole, na wengine kusuasua kutoa maelezo, lakini pia wao wanaelemewa kwasababu hawana hata muda wa kupumzika.
Amesema kuwa wanalazimika kuwaelekeza washike vitu vye ubaridi ili mashine ziweze kuwatambua, jambo ambalo linaongeza uchelewaji wa uandikishaji.


Kwa maelezo ya wananchi hao, wanasema kuwa wamelazimika wengine kufuata chai nyumbani, kwani tangu wameingia kwenye foleni tangu asubuhi, wanashangaa kuona hakuna juhudi za kuonekasha kasi ya kuwafikia lakini wakasema kuwa watavumilia, wasiwasi wao upo kwenye kuisha kwa muda uliopangwa wa may 27 2015.

Uandikishaji ulianza tarehe 21 may 2015 kote mkoani Kagera, ambapo kwa takwimu za kituo cha Kahororo kata, juzi walianza na kuandikisha watu54 jana 22 may wakaandikisha 74 na leo tangu saa2;00 hadi saa 4;30 wameshaandikisha karibia watu 30, na kuonesha kuwa uandikishaji huo hauwezi kukamilika tarehe 27 may zilizopangwa katika maeneo yalioanza.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment