. Ni katika nafasi ya ubunge,
. Ni baada ya wananchi kuomba msaada
wa maabara,
. Asisitiza alifanya makubwa akipewa
atafanya makubwa zaidi.
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgij Dokta Deodoras Kamala wakati akiomba ridhaa hiyo, amesema wananchi waachane na kusikiliza wagombea wanaosema chochote kwa kisingizio cha kupata nafasi za uongozi, kwani baada ya kupata nafasi huwakimbia.
Dokta Deodoras Kamala, amesema hayo alipokuwa akizungumza na
wananchi wa kata Ishozi wilayani Misenyi, akisisitiza kuwa wakati wa kuelekea
uchaguzi mkuu, wananchi ulaghaiwa na kila mwenye kuitaji nafasi ilimradi
akubaliwe na mwananchi.
Amesema kuwa wananchi wanakabiliwa na mambo mengi ya msingi,
lakini wakatio huu wapo wagombea wanaowadanganya wananchi kuwa wapewe nafasi,
ili wakishatawala wapige simu wakati wowote wawasaidie.
Awali diwani wa kata ya ishozi Bwana Alex Tibiita, amemwomba
Balozi Kamala kusaidia ukamilishaji ujenzi wa maabara, akisema kuwa walipofikia
hawataweza kuimalisha kwa wakati, huku akisistiza kuwa wankubali kumpokea akiamua kurejea jimboni.
Kutokana na tatizo hilo, Dokta Kalama amesema kuwa ataongezea
mifuko hamsini ya sementi ili kukamilisha ijenzi wa maabara hizo, huku akisema
kuwa ni vizuri wananchi kukumbuka na kuwa na fadhila na waliyotenda viongozi
waliotangulia.
Akiongea katika kipindi cha redio, mbunge wa sasa anayemaliza muda wake Bi Asumpta Mshama, amesema kuwa ni muhimu wakashiriki pamoja, huku akisema kuwa daraja la Kaja ambalo lilisumbua wananchi kwa muda mrefu, limejegwa na yeye hivyo wasiliite jina la Kmala, japo lilijengwa mwezi mmoja tu baada yake kuwa mbunge.

Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment