. Wananchi wapongeza unjezi baadhi waomba muda,
. Ni fedha kutoka mfuko wa barabara.
Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami umeanza katika kata
Kashai kwa gharama ya mfuko wa Barabara, imetajwa hakuna fidia kwa waliojenga
baada ya kutengwa.

Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita moja inatokea Kashai sokoni kupitia zahanati, Katatorwanso hadi mwisho wa barabara, huku ikishuka hadi mafumbo shuleni, kama anavyofafanua diwani viti maalumu CCM.
Ukarabati huo unafanywa na kampuni ya DECA ENTERPRISE LTD ya mjini Bukoba, ingawa mhandisi wa manispaa ya Bukoba amekuwa mgumu kutoa ufafanuzi, lakini akatujuza kuhusu muda wa kuanza na kumaliza ujenzi huo.
Badhi ya wananchi wamepongeza ujenzi huo, huku wengine wakiomba muda zaidi ili wabomoe maeneo yao wenyewe.
Mchakato wa ujenzi wa barabara hiyo, ulianza mwaka 2013, baada ya kuombewa fungu katika baraza la madiwani wa manispaa ya Bukoba, ambapo harakati za asubuhi imemtafuta mwenyekiti wa CCM wilaya Yusuph Gelvaz Ngaiza.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment