MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday, 9 June 2015

HIKI NDO KIFO CHA MSANII BONGO MOVIE ALFAJIRI LEO.



Ni kifo cha msanii mkongwe wa filamu nchini, Juma Ally Salim ‘Mzee Kankaa’ ambaye amefariki dunia leo alfajiri kule nyumbani kwake Tandale jijini Dar es Salaam, baada ya kutajwa kusumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi kwa muda mrefu.

Mwili wa Mzee Kankaa unatarajiwa kuzikwa leo saa 10 jioni katika makaburi ya Ali Maua jijini Dar es Salaam.

Jama za marehemu wamesema kuwa alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi kwa zaidi ya miaka mitatu sasa,  na kueleza kuwa msiba upo nyumbani kwa marehemu eneo la Tandale-Chama jijini Dar.

Na Mwanaharakati.

No comments: