Jana wafuasi wa CHADEMA WILAYANI Geita
mkoani humo, wamezuia gari la mfuasi ma aliyekuwa katibu wa chama hicho wilaya
Bw Rogers Luhega, baada ya kutangaza kuacha nafasi ya uongozi na kutaka
kujiunga na chama kingine, huku askari polisi aliyejulikana kwa jina mpoja la Zakayo
wa kituo kikuu cha polis Wilaya ya Geita, akiokolewa baada ya kupigwa mara
baada ya kuonekana akirekodi kwa kujificha kwenye mkutano wao uliofanyika
katika viwanja vya soko kuu mjini Geita.
Sakata la kuzui gari la katibu huyo
lilidumu kwa saa2, baada ya wafuasi hao zaidi ya 100 kusikia taarifa kuwa kada
huyo wa CHADEMA aliyetangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Geita amekihama
chama hicho na kwamba alitarajiwa kupokelewa na mjumbe wa NEC CCM Mkoa wa
Geita Leonard Bugomola.
“Tumesikitishwa kweli na taarifa hizi ndio maana tulizuia gari lake lisiondoke mpaka atueleze kama kweli amekihama chama, lakini ametuhakikishia yuko na sisi na tarifa hizo si za kweli, tungeshangaa sana manake juzi juzi hapa tumemchangia fedha za kuchukulia fomu leo hii atugeuke tusingekubali,”alisema Adriani Rwechungula na Ramudi Rasmusi.
Hata hivyo Rogers Luhega
amekanusha madai ya kuwa amekihama chama hicho na kujiunga na chama cha
mapinduzi CCM mbele ya wafuasi hao, kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya
habari na kuhusu kutimuliwa.
“Habari hii ya kujiunga na ccm na
kwamba napokelewa na mjumbe wa nec ccm Mh. Leonard Bugomola si kweli jambo hili
limeleta usumbufu sana watu wananizongazonga kila muda sasa niko mbele yenu
nasema sijahama chama na wala sina mpango wa kuhama na kuhusu kutimuliwa mimi
sijafukuzwa kama ilivyoripotiwa bali niliomba mwenyewe niachie nafasi hiyo ili
nipate muda wa kutosha wa kupambana na ccm kuhakikisha tunalinyakua jimbo la
Geita,”alisema Rogers Luhega.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment