. Nyaraka za
uchunguzi mezani kwa mkuu wa mkoa, baadhi kufukuzwa maslahi ya wananchi,
. Kabla hajarudi
Bukoba mwezi Agost RC atakuwa ameshamaliza kazi,
. Kinana apiga
marufuku kutembelea nyumba za viongozi mara kwa mara,
. Wajumbe wakemea
ujio wake kuwa vidonda badala ya neema.
Ni katika safari ya kuimarisha chama hicho mkoani Kagera, ambapo amekagua miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa katika manispaa ya Bukoba, na kuzungumzia mgogoro uliokuwapo katika chama hicho, huku akisisitiza wahusika kufukuzwa kwa maslahi ya wananchi na kuongeza kuwa watenda maovu wasijiite wana CCM.
Katibu mkuu wa CCM taifa Abdulrahman Kinana amesisitiza wana
Bukoba kukumbuka mambo ya mvutano waliopitia, na kukubali kupokea maamuzi
yatakayotolewa, kwani yatakuwa kwa maslahi ya wananchi wa Bukoba ambao leo
wanataabika na hasa kwa kudhulumiwa, huku akisema kuwa ujenzi wa soko la
gholofa kamwe siyo suluhisho la umaskini kwa wana Bukoba.
Ametolea mfano machinga complex ya Dar es salaam, kuwa
wakati wowote itauzwa kulipa deni, ilhali haijawahi kuwanufaisha wafanyabiasha
kwani wananchi wanatafuta bidhaa chini huku zikiozea juu ya jengo hilo kutokana
na gharama zake na kutoonekana kirahisi kwao
Ni katika mkutano ambao umeudhuriwa na wananchi wa manispaa ya Bukoba waliokuwa na kiu cha kujua mstakabali wa ujenzi mradi wa soko ndipo Kinana akatoa kauli hii.
Katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mayunga
manispaa ya Bukoba, katibu mwenezi CCM taifa ndugu Nape Nnauye, amesisitiza
kuwa kumejengeka desturi ya watu kutumia ofisi kufanya wizi, akisema kuwa hao
ndiyo wachache wanaokichafua CCM , hukua kiongeza kuwa Balozi Kagasheki na
mkakati wake kutetea wananchi wake kunafahamika, na anatosha kwa wakaazi wa
Bukoba
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment