MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday, 6 June 2015

VIDEO; KIFO CHA PADRI NA WANAFUNZI KINASIKITISHA TAZAMA HAPA.



Ni katika ajali ya gari iliyotokea juzi jioni katika eneo la Kigonsera wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma, ambapo Padre Yyasinth Kawonga wa shule ya sekondari ya maketekista Kigonsera na wanafunzi wake walikuwa wakitoka shambani. 

Padre Hyasinth Kawonga ni wa kanisa katoliki jimbo la Mbinga na makatekista 6 waliofariki dunia wawili kati yao ni wanawake na wanne wanaume.

Gari lao gari lenye namba za usajili T306 AYM, liliacha njia na kupinduka kisha kuwaka moto, ambapo majeruhi 24 kati yao waliotibiwa na kuruhusiwa ni 20 na waliolazwa hospital ya Mbinga ni wanne, msichana mmoja na wanaume watatu na gari hiyo inatajwa kutumbukia kwenye korongo lenye urefu wa mita tano na hatimaye kuteketea.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema, peponi, Amen.
 

Na Mwanaharakati.

No comments: