MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday, 4 June 2015

MAMBO YASIYO YA KAWAIDA KATIKA MAZIKO YA MBUNGE WA ZAMANI SAMUEL LUANGISA



. Wapiga picha kuzuiliwa wakati wa salamau za mwisho,
. Utwaliwaji viwanja vya Rugambwa waibuliwa na askofu,
. Watoto wa marehemu waomba Kagasheki awaibie siri aliyomweleza mara ya mwisho.
Maziko ya mzee Samuel Ntabala Luangisa, yamefanyika mtaani kwao Kitendaguro, ambapo alizaliwa 20 jan 1932, na kuzikwa tarehe 3 Jun 2015, ambapo katika maziko hayo, viongozi wa kisiasa, kidini na wananchi walijitokeza na kufanya maziko ya kisasa kupitia kampuni ya Uganda burial Service Ltd.

Walikuwapo waandishi wa habari wa redio, tv na blog mbalimbali, lakini hali ilivyozoeleka ya kupiga picha katika matukio kama hayo, wapiga picha wa Tanzania walizuiliwa kupiga picha badala yake ile kampuni ya mazishi ndiyo ilikuwa na ruksa za kupiga picha wakati wa kutoa salamu za mwisho kwa marehemu.
Itakumbukwa kuwa manispaa ya Bukoba imekuwa na mgogoro wa ardhi baada ya kupimwa viwanja zaidi ya elfu 4 katika kata za Kahororo, Nshambya, na Nyanga ambapo wananchi walilalamika baada ya kukiukwa kwa makubaliano waliyopewa na halmashauri ya manispaa kuwa watafidiwa kwa mujibu wa sheria na kupewa kiwanja kimoja.
Marehemu Ruangisa miezi michache kabla ya kifo chake, kwakushirikiana na Askofu msaidizi jimbo katoliki la Bukoba Dr Method Kilaini, alianza kushughulikia viwanja vya shule ya sekondari Rugambwa, ambavyo hatahivyo halmashauri ya mji wa Bukoba ilimpa Kadinali Rugambwa 1962, lakini manispaa ya Bukoba imeanza kuvimega na kuuza jambo ambalo limekumbushwa na askofu Kilaini kwakuonesha kuitaji msaada wa utatuzi wake
Mtoto wa tisa kati ya watoto 11 wa marehemu Luangisa, Bi Mulungi Kichwabuta, alipata nafasi ya kuzungumza neno la watoto na kutoa shukrani, lakini akasema mbunge wa Bukoba mjini balozi Kagasheki
ambaye alikuwa rafiki wa karibu sana na marehemu, alimtembelea baba yao siku chache kabla ya kifo chake, ambapo marehemu aliwaambia watoto wampishe aongee na balozi, sikiliza alichosema hapa chini
Marehemu Luangisa, alijiunga na TANU baada ya kuacha kazi ya....................
ualimu wilayani Kwimba October 1 1956, badaye alijiunga na CCM 9 Jan 1977 na kupewa kadi namba A 256965, alipata mafunzo ya kisiasa Mzumbe morogoro, China, Corea, Jappan, Uingereza, Uswizi, Ujeruman magharibi na mashariki na alikuwa mjumbe wa halmashauri kuu tangu 1967.

Alikuwa diwani tangu 1975 hadi 2015 mwenyekiti wa halmashauri ya mji na hatimaye meya wa manispaa ya Bukoba, alikuwa mkuu wa mkoa wa kwanza wa Ziwa magharibi na mkoa wa Mara, akawa balozi wa Tanzania China, Corea na Zaire kati ya 1973- 75 na mwaka huo akawa katibu mkuu wa wizara ya jeshi la kujenga taifa.

Na Mwanaharakati.

No comments: