Ni baada ya kuwataka wananchi kuwa makini na watangaza nia wanaoomba
nafasi kupambana na ufisadi ilhali hawana nyezo ya kufanya hivyo.
Amesema kuwa kwa sasa wapo
wengi wanaotafuta nafasi za uongozi, hivyo vyama husika, vipitishe mgombea
kulingana na utekelezaji wake, huku akisema kuwa kisithubutu kupitisha mgombea anayenyooshewa
kidole kwani ni kupoteza haki ya wananchi
Akizungumza katika mdaalo ulioandaliwa na taasisi ya mwalimu
Nyerere mkoani Mtwara, mwanasheria na mchokoza mada Awadh Alli Said, amesema kuwa
wapo viongozi ambao wameshadharau jamii katika nafasi nyingine huku wanajinadi
kuwaongoza katika ngazi za juu zaidi, kuwa huko siyo kujenga amani.
Wakati huo huo Bwana Awadh, amewataka wananchi kutumia
nafasi yao hadimu ya kuchagua, kumchagua kiongozi anayeonesha njia ya kutetea
maslahi yao, kwa kuhepuka wanaotafuta nafasi, huku wakitajwa katika tuhuma za
kudhulumu mali zao.
Mdaalo huo ulioandaliwa na taasisi ya Mwalimu Nyerere, unafanyika katika kipindiu amacho mchakato wa kuwapata wa wagombea kupitia vyama mbalimbali ukiendelea kote nchini, huku baadhi ya watia nia wakifukuzwa na wananchi kama ilivyo katika manispaa ya Bukoba ambapo baadhi ya watia nia wanazomewa na wananchi wakihusishwa na uporaji wa ardhi zao.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment