MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday, 9 July 2015

LIVE UPDATES, KINACHOENDELEA DODOMA

Ni katika kulihutubia bunge la jamhuri ya Muungano, ambapo linavunjwa rasmi tayari kuanza mchakato wa uchaguzi 2015.

Rais sasa anaeleza yaliyotendeka katika uongozi wake akisema kuwa ulinzi umeimarishwa, haki sa binadamu, maadili ya viongozi na mgawanyo wa madaraka.....
Add
Bunge limechangia pakubwa katika maendeleo ya taifa hasa kuanzisha mfuko wa bunge kwa bilioni 123, mfuko wa jimbo ambao ameongeza kuwa lazima uongezewe nguvu.

Anaendelea kusema kuwa kumekuwa na Uhuru wa kisiasa kwa vyama vyote vya siasa na kupata uhuru hata wa kutoka Bungeni, na uchaguzi utafanyika huru kwani ndiyo habari kuu hapa nchini kwasasa, na mchakato umesfanyika na unaedelea ilhali uandikishaji wa watu zaidi ya milioni 11 kupitia BVR.

Anasema kuwa ametanua wigo kwenye sekta ya habari na kuweka uhuru jambo ambalo analaumiwa kwalo lkn hakuna jinsi lazima vyombo vya habari vipate uhuru na kuna vyombo km magazeti zaidi ya 60, redio zaidi ya 100na Tv 29, ilhali serikali ikiwa na gazeti3, resio 1 na tv.

Add..........
Anasema katika miaka 10 kuna kamati za maadili kuratibu maadili yan viongozi ambapo mali na familia za viongozi sasa uangaliwa na kuhakikiwa kazi ambayo inaratibiwa na hazina, pia serikali yake imeimarisha muhimili wa mahakama, kwa kutenganisha shughuli za haki na utawala kwa kujenga ofisi mbili tofauti.

Umeanzishwa mfuko wa mahakama huru na bajeti kutoka bilioni 36 hadi 86, kuongeza idaid ya majaji, wa rufani, mahakama kuu na mahakama za mwanzo, ili kuchangamsha usikilizaji wa kesi, ambapo watu wenye shaada ya kwanza ya sheria wanapata kuteuliwa sasa, na majaji wa rufani kutoka 8 hadi 16, mahakama kuu kutoka 37 hadi 81, na idadi ya wanawake wameongezeka kutoka 8 hadi 37.

Na Mwanaharakati.

No comments: