MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday, 9 July 2015

SERIKALI YATENGA MIKOA, WILAYA, HALMASHAURI NA MANISPAA

SERIKALI imegawanya mkoa wa Mbeya na kupata mkoa mpya wa Sogwe, wilaya mpya sita, halmashauri 25, Manispaa 17 na tarafa tano kata 586 nchini.

Akihitimisha Bunge la kumi, Mkutano wa 20, jana mjini Dodoma, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema mgawanyo huo umetokana na Rais Jakaya Kikwete, kuridhia kugawanywa kwa maeneo hayo mapya ya utawala.

Alisema lengo la mgawanyo huo ni kusaidia kusogeza utawala na usimamizimwa shughuoi za maendeleo karibu na watu, na kwmaba zipo ambayomyapo chini ya mamlaka ya Rais na waziri mwneye mamlaka na serikali za mitaa.

Pinda alizitaja wilaya mpya kuwa ni Tanganyika, Ubungo, Kigamboni, Sogwe, Kibiti na Malinyi
Alizitaja Halmashauri mpya kuwa ni Buchosa, Malinyi, Madaba, Manyoni, Mpimbwe, Msimbo, Mlele, Buhigwe, Kakonko, Uvinza, Kyerwa, Chemba, Mbogwe, Nyang'wale, Butiama, Momba, Nyasa, Bushetu, Busega, Itilima, Ikungi, Mkalama, Msalala, Kaliua na Bumbuli.

Pinda alitaja Miji na Manispaa kuwa ni Chalinze, Ifakara, Nanyamba, Newala, Kondoa, Mafinga, Mbulu, Bunda, Mbinga, Tunduma, Handeni, Nzega, Kasulu, Geita, Masasi, Ilemela na Kahama.

Pia kuna tarafa moja ikiwa wilaya ya Newala ambayo ni mchemwa, nyingine nne zipo wilaya ya Tandahimba, Mchichira, Mwihambwe, Mabamba na Mangombiya.
 
Alisema serikali itaweka mfumo imara na usimamizi madhubuti ikiwamo, na maafisa masuhuru wanashauri kubana matumizi hasa katika ununuzi wa umma, kudhibiti uendeshaji wa semina zisizo za tija, ununuzi wa magari, gharama za kutaufa, msimu, umeme na maji.

Na Mwanaharakati.

No comments: