MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday, 5 August 2015

MAKUBWA BAADA YA MWENGE WA UHURU KUTUA KAGERA HAYA HAPA



Mwenge wa Uhuru kuzindua miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 13 mkoani Kagera ambapo Mwenge huo ulipokelewa mkoani hapa Wilayani  Biharamulo Kata ya Kalenge mpakani na Mkoa wa Kigoma tarehe 2/08/2015.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella  akipokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Issa Machibya alisema kuwa Mwenge wa Uhuru utakimbizwa mkoani Kagera katika Halmshauri zote za Wilaya saba na Manispaa ya Bukoba na kupitia jumla ya miradi 52.

Katika miradi hiyo 52 Mwenge wa Uhuru utazindua miaradi 25, utakagua miradi 12, utaweka mawe ya msingi katika miradi 13 aidha  Mwenge huo  utapitia miradi mingine miwili ya kijamii ili kuhamasisha maendeleo kwa wananchi wa mkoa wa Kagera.

Mhe. Mongella alitaja mchanganuo wa gharama za miradi hiyo 52 itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru kuwa serikali kuu imechangia kiasi cha shilingi 3,257,174,146 sawa asilimia 23.8 Halmashauri za Wilaya zimechangia  kiasi cha shilingi 1,763,070,553 sawa na asilimia 12.9.

Aidha wananchi wamechangia  shilingi 3,086,502,508 sawa na asilimia 22.5  wahisani wamechangia shilingi 5,595,751,962 sawa na asilimia 40.8  ambapo jumla ya gharama yote katika Halmashauri za Wilaya na Manispaa ya Bukoba katika mkoa wa Kagera ni shilingi 13,702,499,169 sawa na asilimia 100.
Mwenge wa Uhuru wenye ujumbe  usemao Tumia Haki yako ya Kidemokrasia, Jiandiishe na kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa 2015, Vijana wa leo na UKIMWI wazazi tuwajibike, Uteja wa Dawa za kulevya unazuilika na kutibika chukua hatua, Wekeza kwa maisha ya baadae tokomeza Malaria, pia Kata mnyororo wa Rushwa  chagua kiongozi mzalendo.
Ujumbe huo unalenga kuwahamasisha wananchi hasa vijana kujikita katika shughuliza uzalishaji badala ya kujihusisha na madawa ya kulevya, uteja, ngono zembe, rushwa  pia na kuchukua hatua dhidi ya malaria pia wananchi kujitokeza kujiandikisha na kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu 2015.
Mwenge waUhuru ulipokelewa Wilayani Biharamulo tarehe 2/08/kuelekea Biharamulo ni Ngara, Kyerwa, Karagwe, Misenyi, Bukoba Vijijini, Manisapaa ya Bukoba na mwisho ni Muleba na Mkoa utakabidhi Mwenge mkoa wa Geita.
Mwenge wa Uhuru uliopokelewa tarehe 2/08/2015 unatarajia kumaliza mbio zake mkoani Kagera tarehe 9/08/2015 na kukabidhiwa mkoani Geita tarehe 10/08/2015 aidha utahitimisha mbio zake kitaifa mkoani Dodoma tarehe 14/10/2015 na kukabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete.
 

Na Afisa habari mkoa.

No comments: