MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 2 August 2015

MATOKEO YOTE KURA ZA MAONI KAGERA BAADHI KUTOLIPA HELA ZA MIKUTANO

Katika upigaji wa kura mkoani Kagera, wana CCM wamechagua wagombea watakaopeperusha bendera ya chama hicho katika kampeini za 2015 katika majimbo mbalimbali.

Bukoba mjini wagombea walikuwa nane, ambapo balozi Kagasheki ameshinda kwa kura 6971, akifuatiwa na Amani aliyepata kura 944.
Bukoba vijijini mshindi ni Jacson Rweikiza, Muleba kaskazini Mwijage, Muleba kusini Profesa Anna Tibaijuka, Nkenge Dr Diodorous Kamala kura 8,229 dhidi ya Kyombo 5,429 na Assumpta Mshama 5,273.

Katika manispaa ya Bukoba kabla ya kutangza matokeo, mkurugenzi wa uchaguzi CCM ambaye pia ni katibu wa chama wilaya, amesema kuwa Dr Amani hakujitokeza kusaini lakini alipotafutwa alitoa udhulu, hivyo leo subuhi ametakiwa kusaini kwasababu ndiyo sheria za chama wala siyo ihali.
Mtandao huu bado unafuatilia taarifa za watia nia watatu katika manispaa ya Bukoba walioshindwa kulipa milioni 2 za kampeini kwa mujibu wa kanuni za chama, ambao ni Mjuni Kataraiya, Anatory Amani na George Lubaiyuka.
Na Mwanaharakati.

No comments: