MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday, 7 August 2015

MAKUBWA; TAKUKURU KAGERA YACHUNGUZA TAARIFA ZA RUSHWA KURA ZA MAONI.



. Matukio 31 yachunguzwa na TAKUKURU,
. Upotoshaji wahusishwa,
. Wanahabari waaswa kuwa makini.

Akizungumza na mtandao huu juu ya malalamiko ya wananchi kwa kutaja RUSHWA kwa kila jambo mkoani Kagera, mkuu wa TAKUKURU Kagera RBC Joseph Mwaiswelo, amesema kuwa imekuwa ngumu kukomesha rushwa kama hakuna mlalamikaji kati ya mtoaji na mpokeaji.

Matukio 31 kuchunguzwa TAKUKURU;-
Mwaiswelo amesema matukio 31 yamethibitishwa, ambayo hatahivyo bado yanachunguzwa kwa kuwahoji watoa taarifa, lakini bado hakuna lililokwisha muhusisha moja kwa moja anayetajwa kutoa au kupokea rushwa, kwasababu wanaotajwa kutoa hongo ni waliotia nia za kugombea ambao amesema huwezi kuwahoji kabala hujawa na uhakika wa kilichotajwa.

Kuhusishwa upotoshaji;-
Katika kipindi cha kampeini hadi upigaji kura ya maoni kuelekea kupata wagombea wa udiwani na ubunge katika majimbo yote ya mkoa wa Kagera, TAKUKURU imepokea taarifa nyingi za uongo, hasa ambapo mtoa taarifa hasa kwa njia ya simu anapotakiwa kuongozana na afisa na kushindwa kufanya hivyo.

Wanahabari waaswa kuwa makini;-
Kutokana na baadhi ya maswali kwa wanahabari kuonekana kuegemea sehemu au kwa mtu, afisa huyo wa TAKUKURU mkoa amewataka waandishi hao kuwa makini, kutokubali kutumika na baadhi ya watu ili kuwachafua wenzao, ilhali akisisitiza kuwa chombo cha habari kinatangaza au kuandika kupitia sera ya chombo hicho na malengo ya mmiliki kama alivyoruhusiwa na mamlaka, hivyo kuna haki zinazomlinda.
Katika mkutano huo, baadhi ya wanahabari wameonekana kulazimisha kupata majibu ambayo hayawezekani kwa mujibu wa sheria na taratibu, kwani hayaendani na baadhi ya maswali yaliyoulizwa wala hayahusiani na rushwa, hivyo kuwataka kujua kanuni za taasisi husika kabla ya kuwatuhumu wahusika wake.


Na Mwanaharakati.

No comments: