MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 23 August 2015

MAZITO KATIKA UZINDUZI KAMPEINI ZA CCM JANGWANI DAR ES SALAAM.

Viongozi na waasisi wa CCM wameudhuria na kuongea mazito, pamoja na mwenyekiti wa sasa Mh Jakaya Kikwete, marais wastaafu Ali Assan Mwinyi, na Benjamin Mkapa , makamu wa rais Gharib Bilali na waasisi wengine wa chama hicho kama Jaj Warioba, Yusuph Makamba na mtoto wa Mwl Makongoro Nyerere na wengineo.

Makundi mbalimbali yamejitokeza na kueleza mapendekezo yao ambapo miongoni mwa waliowakilisha ni mwenyekiti msaidizi wa machinga mkoa wa Dar es salaam , mwenyekiti wa shirikisho la watu wenye ulemavu Tz na mwenyekiti wa bodaboda.
Jaji Joseph Sinde Warioba; amewaeleza watanzania kuhusu sifa za wagombea wa CCM kuwa chama kimetazama sifa tatu, uchapa kazi, uadilifu na uzalendo.

Amesema kuwa ukizungumzia uchapakazi wa magufuli ni lazima uutazame katika vipindi vitatu alivyoudumu katika wizara kadhaa hasa ya ujenzi ambayo imeiunganisha Dar es salaam na mikoa yote Tanzania kwa barabara, akifanya kazi ndani na nje ya serikali.
Jaji huyo mstaafu, amesema kuwa alipewa kazi na rais mkapa katika awamu ya tatu, ambapo alikuwa akichunguza rushwa na kugundua ufisadi mkuu ulikuwa katika ujenzi ambapo katika kipindi cha miaka 20 tangu kuchunguza, Magufuli ameingia katika wizara hiyo kwa miaka 15 sasa na hakuna tena taarifa za ufisadi katika ujenzi kama ilivyokuwa awali.
Chanzo kikuu cha ufisadi, amekitaja kuwa ni kukaa karibu kwa viongozi na mafisadi, kwani taifa lina matatizo ya kuporomoka kwa maadili ambapo kiongozi bora anatakiwa kuwa mzalendo bila kuwa na makundi ila kundi moja ambalo ni watanzania.

Ameongeza kuwa mabadiliko yanayotajwa na baadhi ya watu tayari yamefanywa na CCM kwa kiasi kikubwa kwa mara ya kwanza baada ya kuweka wagombea wenye sifa hizo tatu na kubwa zaidi kumweka mwanamke kama makamu wa Tanzania.

Rais wa Zanzibar na mwakilishi wa baraza la mapinduzi;  Dr.Ali Mohamed Shein
amesema kuwa ni wakati wa watanzania kuenzi kazi kubwa iliyofanywa na Magufuli, na wazanzibar wanayatambua, wakatuma salamu zao ili kudhiilisha ukweli wao, akisisitiza kuwa uongozi siyo wa kujaribu hiyo watanzania wawe makini.






Rais mstaafu wa awamu ya pili; Ali Assan Mwinyi amesema kuwa upinzani ni muhimu na upo siku nyingi lakini siku imefika wao kuazima viongozi na dhamira ya waliokwenda wameenda kuongeza nguvu ili kuishinda CCM lakini yawezekana ikawepo CCM mbili A na B.

Rais wa awamu ya tatu; Benjamin Willaim Mkapa, amesema katika hao nane walioteuliwa na tume ya uchaguzi, watanzania watazame timu bora kwasababu ndiyo itasukuma maendeleo yao lakini watambue kuwa hapa nchini kuna chama kimo tu cha ukombozi, huku akikumbusha sifa za viongozi madhubuti kuwa ni wale wanaotekeleza imani za wananchi kwa vitendo, kushiriki na wenzao, kuwa mstari wa mbele kutekeleza mambo ya umma kupitia ccm, wakati wote mfano kauli zao na mtazamo wao kwa kutokuwa wazululaji.

Haitoshi kusema tu kuwa unachukia umaskini bali masharti na taratibu za kuondoa umaskini.

No comments: