Nkumba alipojitoa CCM alisema
alikipenda kwa dhati chama hicho lakini hakuona sababu ya kuendelea kubaki kwa
kuwa hasikilizwi na hakina mapenzi na watu.
Ni aliyekuwa mbunge wa Sikonge, kupitia
CCM, ambapo alihama chama hicho hivi karibuni baada ya upepo wa Lowasa kuvuma
CHADEMA, sasa amerejea kwenye chama chake akisistiza kuwa alikosea njia.
Alikuwa amejiunga CHADEMA baada ya
kushindwa katika kura za maoni kugombea ubunge wa Sikonge, akawa ameteuliwa na
CHADEMA kugombea nafasi hiyo lakini wanachama wa chama hicho walinung’unikia
kamati kuu ya CHADEMA kwa kumteua badala ya Hija Ramadhan, ambaye alirudishwa
na kusababisha Said Nkumba kurejea CCM.
Akizungumza na wanahabari Dar es salaam,
Nkumba amesema ameamua kurejea nyumbani CCM kwani alikipenda CHADEMA ila
amegundua hakina mwelekeo, ambapo imemlazimu kurudi kwenye tawi lake la CCM
kuomba upya kadi kwani hakuna tatizo kurejea, hayo yakiwa ni maneno ya katibu
wa CCM wilaya ya Sikonge Seleman Majilanga.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment