Akuzingumza na mtandao huu, mratibu uchaguzi manispaa ya
Bukoba amepokea mapingamizi 10 kutoka kata mbalimbali katika ngazi ya udiwani.
Mapingamizi hayo yamewekwa na wagombea udiwani katika vyama
mbalimbali vya siasa, ambapo mratibu wa huyo wa uchaguzi Bw Elick Bazombopora,
amesema kuwa mgombea wa kata Kahororo Bw Chief Abdronicas Kalumuna amewawekea
mapingamizi wagombea Venant Lugemalila
Salapion wa CCM na Bnyenza Saimon wa ACT, hatahivyo Bw Banyeza amepeleka pingamizi ambalo haliokutaja linampinga
nani.
Mratibu huyo amesema kuwa katika kata Miembeni Pingamizi
limewekwa na Baganda Gyeshumba Richard wa CHADEMA akimwekea Richard Gasper,
ambapo katika kata Kashai, mgombea wa
CCM Bw Samora Agaptus Lyakurwa, amewekea pingamizi ndugu Kabaju Abdukad, ilhali
katika kata Kagondo kuna mapingamizi matano na mapigamizi matatu yakiwekwa na
Anatory Aman kwa wagombea watatu.
Amesema kuwa amewawekea Simart Peter Baitan wa CCM, Joram
Ifunya wa CHADEMA, na tatu kwa mgombea wa ACT Benson George Bitegeko, ambapo
Joram wa CHADEMA amemwekea Baitan wa CCM, ilhali Benson George Bitegeko akimwekea Anatory
Amani.
Katika barua yake yenye kumbukumbu namba BMC/KT/KAG/A.2/49,
amabaye ni msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata Kagondo, amesema kuwa ametengua
uteuzi wa Dr Anatory Amani kugombea udiwani, kutokana na pingamizi la Bw Benson
George Bitegeko wa ACT kuhusu kudanganya eneo alilozaliwa, ambapo katika barua
yake Amani alionesha kuzaliwa wilayani Karagwe, ilhali taarifa za mamlaka
zinaonesha amezaliwa katika eneo la Kanoni Ruanda, kwenye wilaya ya Rakai
nchini Uganda, hivyo hakutoa taarifa sahihi za kuzaliwa kwake.
Kupitia baraua yenye kumbukumbu KSH/UCH/VEO.1/05,
iliyoandikwa na msimamizi kata Kashai, imetengua uteuzi wa ndugu Kabaju
Nuruhuda Abdukadir kugombea udiwani kwenye kata hiyo kwasababu ya pingamizi
alilowekewwa na mgombea wa CCM ndugu Samora Agapmtus Lyakurwa.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment