Katika
awamu ya tatu ya mfuko wa kaya maskini nchini, mkoani Kagera wameendelea na
utaratibu wa ugawaji fedha katika kaya husika, ambapo jumla ya mil 319,060,000/=
zinazotolewa kwa walengwa 8753 Bukoba
vijijini, na kiwango cha chini ni sh 20,000/= ilhali cha juu kikiwa ni sh
86,000/= kulingana na ukubwa wa familia.
Mtandao
huu umeshuudia mchakato wa utoaji fedha kwa baadhi ya kaya kwenye kata za Bujugo na Karabaige, kando na hiyo
kumekuwa na malalamiko juu ya mfuko huo, ikitajwa kuwa wanaopewa siyo wahusika
yaani ni wale wanaojiweza na wasio jiweza kuwekwa kando.
Ismail Hamidu ambaye ni afisamratibu wa TASAF
halmashauri ya Bukoba vijijini Bw Ismail, amesema kuwa wao hawahusiki kufanya mchakato wa utambuzi kuhusu maskini,
badala yake ni viongozi wa vitongoji na mitaa ambao wanaishi karibu na
wahusika, ambapo taarifa zao ndizo zinawezesha kuwapa mgawo sawa kulingana na
ukubwa wa kaya.
Amesisitiza kuwa TASAF haihusiki kutambua kaya maskini bali ni kazi ya wanavijiji au mitaa husika na wao hupewa taarifa baada ya kukidhi vigezo vinavyotolewa na TASAF, hivyo malalamiko yanayojitokeza siyo ya msingi.
Amesema
kuwa awali kulikuwa na wakati mgumu kuwapata wahusika, kwasababu kulikuwa na
uvumi kuwa fedha hizo ni za FREEMASON lakini baada ya kugundua siyo kweli,
wamejikuta wakitaka kuingizwa kwenye mchakato ilhali hawakuudhuria mikutano ya
utambuzi, ndiyo maana kuna baadhi ya malalamiko kuwa wamebaguliwa.
Kaimu
mkurugenzi wa halmashauri ya Bukoba Bi Jenista Lugakingira, amesema kuwa serikali
inaendelea kutekeleza mipango yake kwa wananchi, kwani inatambua umuhimu na
mahitaji katika kusukuma mbele maisha yao, huku akiwasihi kujitokeza kupiga
kura kumchagua kiongozi wanayemtaka, ifikapo oktoba 25 mwaka huu.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment