Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini
Tanzania, Francisco Montecillo akiwa
ofisini kwa Mkuu wa Mkoa Kagera ameshukuru
serikali ya mkoa wa Kagera kwa kuwaunganisha wananchi wa Kagera bila kujali imani zao ambapo wanafanya
shughuli zao kila mmoja kwa imani yake
bila usumbufu wowote.
Pia Balozi Padilla alisema kuwa serikali
inafanya kazi moja ya kuwaudumia wananchi pia na dini zinafanya kazi ya
kuwahudumia wananchi hao hao kiroho kwa hiyo hakuna haja ya serikali na dini
kugombana wala kukwaruzana kwasababu wote wanafanya kazi moja kwa wananchi.
“Ni bora kuendeleza ushirikiano uliopo
kati ya serikali na dini na nashukuru jambo hilo linatekelezwa mkoani Kagera, nimekuja
kukagua shughuli mbalimbali hapa na kupata baraka za pamoja na wakristo wa mkoa
wa Kagera ili kujenga jamii moja yenye familia moja katika kumtukuza Mungu.”
Alimalizia Balozi Padilla.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera John Mongella
akimkaribisha Balozi Padilla alimshukuru kwa kufanya ziara mkoani Kagera na
alimweleza kuwa serikali inatambua juhudi za kanisa Katoliki katika kuleta
maendeleo kwa wananchi hasa ujenzi wa shule na hospitali kama huduma za jamii
kwa wananch,i pia kutoa huduma za kiroho zinazosaidia kukuza maadili katika
jamii.
Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa
chini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla ziara yake imeanza leo Septemba 3,
2015 na anatarajia kuwepo mkoani hapa kwa takribani siku sita, aidha Balozi
Padilla anatarajiwa kuongoza ibada takatifu ya maombezi ya Bikra Maria katika
hija huko Nyakijooga Parokiani Mugana Wilayani Missenyi tarehe 6.09.2015 siku ya Jumapili.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment