MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 7 September 2015

MUGEZA VIZIWI HATARINI, YAOMBA MSAADA WA MBUNGE



. Ufinyu wa luzuku kwa wafadhili,
. Ukosefu wa motisha kwa watenda kazi,
. Yakabiliwa na deni la milioni 50.
Kandayaziwa blog imetembelea shule hiyo inayojulkana kama Mugeza viziwi iliyoko
Bukoba mkoani Kagera, inayotunza watoto 120 wenye ulemavu wa usikivu na kuongea, na kufanya mazungumzo na mwalimu mkuu wa shule hiyo Hosea Kato, aliyefafanua kuwa wanauhitaji wa walimu 6 ili kukamilisha idadi inayoendana na idadi ya wanafunzi hao.





“Tunajitahidi kuwapa tiba wale wanaopokelewa wakiwa wagonjwa, lakini pia tunaweza
kutoa ushauri kwa tunaobaini kuwa wanaweza kupona” hiyo ni kauli ya Dr Amin Said ambaye ni daktari wa watoto wanaopokelewa katika shule hiyo.






Shule ya Mugeza viziwi ndiyo shule pekee kanda ya ziwa, kutoa huduma na kufundisha watoto wenye ulemavu wa kusikia na kutoongea, ambapo kwasasa ina wanafunzi 120 ilhali idadi hiyo haiongezeki kutokana na mwamko mdogo wa wazazi kuwapeleka watoto wao shuleni hapo.


Na Mwanaharakati.

No comments: