.
Kagasheki siwezi kupoteza muda kujadili matusi,
.
Rwakatare asema naye alete mke wake,
.
Wapambe wa Lowasa wamkana.
Mikutano miwili imefanyika katika
manispaa ya Bukoba ikihusisha CCM na UKAWA, ambapo katika uwanja wa mashujaa
Mayunga, rais mstaafu Benjamin Mkapa, ameongoza wanaccm kuzindua kampeini za
chama hicho mkoani Kagera.
Kwa niaba ya wagombea ubunge ccm katika
mkoa wa Kagera, Bw Mwijage ambaye anagombea jimboni Muleba, amesema kuwa
waliokuwa wanachafua ccm wameondoka baada ya kunyimwa nafasi na wengine
wamefukuzwa, hivyo wameamua kuleta mabadiliko ya kweli kwasababu waliokuwa
wakikwamisha ndiyo walioondolewa.
Balozi Kagasheki, amesema kuwa baada ya
uzinduzi uliofanyika, atafanya kampeini kwa kuzungumzia matatizo yanayowakabili
wananchi, kwani waliokuwa wanaleta shida wameondoka na hayuko tayari kujibizana
nao kwasababu majibizano na matusi, siyo utatuzi wa matatizo ya wanyonge.
Kwa upande wao UKAWA kupitia mgombea
ubunge Wilfred Muganyizi Rwakatare, amesema kuwa wapewe nafasi nyingine kwani
aliwahi kuwa mbunge wa jimbo hilo, ila akipata nafasi anaweza kufanya vizuri
kwasababu ameshajifunza.
Wapambe wa mgombea huyo kupitia UKAWA,
wamesema kuwa wanapanda jukwaa kumshughulikia Kagasheki pekee kwa kutaja mambo
mbalimbali binafsi yanayomuhusu mgombea huyo kupitia CCM.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment