Msemaji wa
polisi ni miongoni mwa wale waliofutwa kazi kulingana nataarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari nchini humo.
Tume ya huduma
za maafisa wa polisi iliwafuta kazi maafisa hao baada ya kuwakagua maafisa
1,300 kwa kipindi cha miezi 14.
Mbali na msemaji
wa kikosi cha polisi wa utawala Masoud Mwinyi,wengi wa wale waliosimamishwa
kazi wanatoka katika idara ya trafiki.
Mwenyekiti wa
tume hiyo Johnston Kavuludi amesema kuwa wakati wa ukaguzi huo waligundua
kwamba maafisa wa vyeo vya chini wanaofanya kazi katika idara hiyo walikuwa
wakituma kiwango cha fedha wanachopata kwa maafisa wanaowasimamia kupitia simu
zao.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment