Baraza
la Vyama vya Siasa nchini limevishauri vyama vya siasa kuzungumza na kuwasihi
wafuasi wao kutii sheria bila shuruti ili kuendeleza amani iliyopo nchini.
Aidha
Baraza hilo limeviomba Vyama kuwaeleza wafuasi na wapenzi wao kurudi majumbani
na kuendelea na shughuli zao mara baada ya kupiga kura siku ya uchaguzi mkuu
kama ilivyokuwa kwa hatua za uandikishwaji.
Hayo
yameelezwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Peter Kuga Mziray wakati
alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu Kikako maalumu cha Baraza
hilo kilichofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.
Kikao
hicho kilitafakari mwenendo wa Kampeni za Wagombea katika ngazi mbalimbali na
kujadili changamoto mbalimbali na utatuzi wake ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa
huru na haki na kufanyika katika mazingira ya Amani na Utulivu.
Mziray
amefahamisha kuwa wamekubaliana katika kikao hicho kuwa Wapiga kura wana haki
kama watapenda mara baada ya kura kuhesabiwa na matokeo kubandikwa kwenda
Vituoni hapo kwa ajili ya kuangalia Matokeo kwa wakati wanaopenda.
Aidha
amesema Vyama pia vimesisitizwa kuweka Mawakala wanaowaamini katika Vituo vya
kupigia kura ambao watajumuisha kura za Wagombea katika nafasi za Madiwani,
Wabunge na Rais katika maeneo husika.
Mziray
ameongeza kuwa Baraza la Vyama vya siasa pia limeshauri Vyama hivyo kuzingatia
na kuweka amani ya nchi mbele kwa maslahi ya Taifa.
“Katiba
ya Nchi iko wazi kuwa atakayeshinda kwa kura nyingi ndiye atakayetangazwa na
kupewa cheti na Tume ya uchaguzi” alisema Mziray
Ametoa rai
kwa Katibu Mkuu kiongozi kuratibu shughuli za kuapishwa Rais ambaye kwa mujibu
wa Sheria huapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania mara baada ya kutangazwa ndani ya
kipindi kisichozidi siku saba.
Mzirai pia
ameelezea kufarijika kwao na Tume ya Uchaguzi kwa kuvihakikishia Vyama vya
siasa kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki na kwamba Mgombea atakayeshinda kwa
kura nyingi zaidi na halali ndiye atakayetangazwa kuwa Mshindi.
Mzirai
amevimetaka Vyama vya siasa kuwaasa Wagombea wao kukubali Matokeo kama
yatakavyotangazwa na Tume ya uchaguzi ya kushinda au kushindwa.
Kwa
upande wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mwenyekiti wake Jaji Mstaafu Damian Lubuva
na Mwakilishi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Khamis Khamis wakati
wakiwasilisha mada juu ya usimamizi na utekelezaji wa maadili Uchaguzi nchini
wamevitaka Vyama vya sias kuendelea kuzingatia maadili ya uchaguzi kwa kuwa
shauku ya kila Mtanzania ni kuona uchaguzi unaisha kwa amani.
Kikao hicho
maalum cha cha siku mbili cha Baraza la Vyama vya Siasa kilijumuisha Wajumbe
kutoka Baraza hilo, Wageni kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar ZEC na Jeshi la Polisi na kuandaliwa na Ofisi ya Msajili
wa Vyama vya siasa nchini.
Baraza la
Vyama vya Siasa limeundwa chini ya kifungu 21B cha Sheria ya Vyama vya siasa
Namba 5 ya mwaka 1992 kama ilivyorekebishwa na Sheria namba 7 ya mwaka
2009.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment