Mtu
mmoja ameangukiwa na mawe na kufukiwa na kifusi cha mchanga katika milima ya Rwome
kata ya kashai manispaa ya bukoba na kupoteza maisha hapo hapo.
Akizungumza
na mtandao huu, mwenyekiti wa mtaa huo bwana PONSIAN WAMALA amesema kuwa katika
shimo hilo alikuwemo vijana watatu ambapo wawili wamenusurika huku mmoja
akipoteza maisha.
Bwana
wamala amentaja aliyepoteza maisha kuwa ni ARISTIDES SEVELINI mkazi wa mtaa huo
ambapo mwenyekiti amesema kuwa hakuacha mke wala watoto.
Amesema
kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa sita mchana ambapo vijana hao walikuwa
wakiendelea na shughuli zao za kuchimba mchanga.
Bwana
Wamala ameongeza kuwa kutokana na tukio hilo serikali ya mtaa imeamua kufunga
maeneo hayo ili yasilete madhara zaidi.
Vikosi
vya uokoaji vya zimamoto na polisi mkoa, vimesaidia kuchimbua mwili wa marehemu
na kuupeleka chumba cha kuifadhia maiti mjini Bukoba kwa taratibu zaidi.
Akiongea
katika mkutano wa hadhara mgombea ubunge kupiti CCM Balozi KHAMIS KAGASHEKI ametoa pole kwa
familia ya marehemu.
Balozi
Kagasheki amesema kuwa yuko pamoja na familia ya kijana huyo katika kipindi
hiki kigumu.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment