Kufuata ugumu wa maisha unaoendelea
kumkabili bibi Zainabu Lipuga aliyekuwa akiishi juu ya dari na mjukuu kwa
muda wa miaka mitatu sasa ameanza kuponda kokoto ili kujikimu huku.
Mwandishi wa mtandao huu amemtembelea
kuangalia maendeleo yake na kukuta bibi huyo, alisema kuwa ugumu wa maisha
umepelekea apate shida kupata matibabu kwake na mjukuu wake.
Alisema kuwa kwasasa
anajishughulisha na upondaji wa mawe ili kuuza kokoto ambazo zimekuwa zikimpa
wakati mgumu kutokana na umri kuwa mkubwa hivyo kupata maumivu mara kwa mara.
“Sio kwamba hizi kokoto ndio
ambazo zinanisaidia hapana hizi zinaniongezea maumivu ya kifua na pia natumia
nguvu nyingi kuponda wakati nauza kwa bei ndogo sana….
“Hali ya mjukuu wangu ndio
inanifanya ni hangaike ili angalau apate chakula asilale njaa ila nasikitika
sana ninanpoondoka kwenda kutafuta riziki lakini nikipata mfadhiri akamletea
mjukuu wangu kiti nitafarijika sana kwakuwa atakuwa na uwezo wakukaa na mimi
nje wakati naponda mawe kwakuwa ndio yanayotusaidia kuingiza kipato katika maisha
yetu” alisema Lipuga
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment